Afisa Habari wa ngazi ya
kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo
akiwakaribisha waandishi wa chama cha habari za Mazingira Tanzania (JET) na
kuwatambulisha wazungumzaji katika mkutano wa taarifa fupi katika kuwapa mwanga
kuhusu yatokanayo na taarifa ya mabadiliko ya tabianchi uliofanyika Doha.
Katikati ni Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro na kushoto Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi.
Mkutano huu uliowakutanisha
pamoja waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) umeratibiwa na Kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam
kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo.
Mtaalam wa Mazingira wa
UNDP Bw. Amani Ngusaro akielezea kwa ufupi jinsi Umoja wa Mataifa
unavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya
Tabianchi na kufafanua Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana
na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI)
unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumzia
yatokanayo mkutano wa mabadiliko ya tabianchi ikiwemo swala la Gesi joto ambapo
amesema kwa nchi kama Tanzania haichafui mazingira kulinganisha na nchi
zinazoendelea zenye viwanda vikubwa pamoja na makubaliano waliyofikikia katika
mkutano huo ambayo yatatolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira hivi karibuni.
Mmoja wa waandishi wa
habari Bi. Judica Laswai kutoka TBC akieleza namna alivyoweza kupata nafasi ya
kuhudhuria mkutano wa mabadiliko ya tabianchini uliofanyika Doha hivi karibuni
kwa kushiriki mashindano ya kuaanda vipindi vya mazingira na mwishowe kushinda
safari iliyodhaminiwa ni Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC)
ambapo amewahimiza wanahabari wenzake kutumia fursa za mitandao ya
kijamii.
Pichani Juu na chini ni
baadhi ya waandishi wa habari za Mazingira (JET) wakiuliza maswali na kutoa
maoni kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi (hayupo pichani).
Pichani Juu na Chini ni
baadhi ya waandishi wa habari wa Mazingira (JET) waliohudhuria mkutano
huo.
Afisa habari Ngazi ya Taifa
wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma akitoa
changamoto kwa waandishi wa habari wa mazingira kuzipa kipaumbele habari za
mazingira na kuwataka kuweka usawa katika habari wanazoandika.


Post a Comment