Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi.
*****************************
Na
Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Watu wanne wa Kundi la “lambalamba”
wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Dodoma
kwa kijifanya wanafichua wachawi katika vijiji mbalimbali katika maeneo
ya wilaya za Chamwino, Kongwa na Mpwapwa. kumbe wanawatapeli wanavijiji kwa
lengo la kujipatia fedha
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa Jeshi la
Polisi Bw. David Misime amesema uchunguzi wao umebaini kuwa vitu wanavyojifanya
kuvitoa ndani ya nyumba au maduka ya watu, kuwa ni wao wenyewe hutuma wenzao
kuvipandikiza na baadaye hujifanya wamevikuta kwenye nyumba ya mtu
anayetuhumiwa kuwa ni mchawi.
Aliwataja
waliokamatwa wakiwa wanajiandaa kuendesha shughuli za lambalamba katika kijiji
cha Vilundilo Wilayani Kongwa kuwa ni mwanaume mmoja Mkombozi Salehe, na
wanawake watatu ambao ni Hadija Tupa, Joyce Nhembelo
na Siwema Kwaeli, ambao walikuwa ni kwa ajili ya kuwapikia
lambalamba hao.
“Wanawake
waengine hutafutwa kwa ajili ya kulala nao jambo ambalo ni hatari kwani mbali ya
kwamba ni kinyume cha sheria na unyanyasaji wa kijinsia pia upo uwezekano mkubwa
wa kuambukizwa magonjwa ikiwepo UKIMWI.” Alisisitiza Bw. David
Misime
Aidha
alitoa wito kwa wananchi kuelewa kuwa wanatapeliwa fedha zao na
hao watu waliobuni mradi wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwani
wamejionea wenyewe kuwa wanachangishwa fedha kabla ya kuwaita na hata wanaodaiwa
kuwa wachawi, hudaiwa kiasi cha fedha.
Kamanda
David Misime alisema kuwa shughuli wanazoendesha kundi hilo la Lamba lamba ni
kinyume cha sheria za nchi na ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binanadamu kwa
kuwaita baadhi ya watu kuwa ni wachawi kwa lengo la kujipatia
fedha.
Mkuu
huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma alisema Upelelezi zaidi unakamilishwa ili
wafikishwe mahakamani wakati wowote, pamoja na Ufuatiliaji wa
lambalamba wengine waliokimbia pamoja na viongozi vijiji wanaoshirikiana nao
unaendelea.
Wakati
huo huo Polisi Mkoani Dodoma inamshikilia kwa mahojiano IDDI S/O
RAMADHANI PANDAUYAGA @ NGOSHA, MSUKUMA, Mkazi wa DODOMA MAKULU baada ya
kulalamikiwa na wananchi wengi kwa kujipatia fedha kwa njia udanganyifu kuwa
anawauzia viwanja.
Kamanda
Misime amesema hadi sasa mtu huyo ameshatapeli zaidi ya Tshs. 24,537,000/=
kuanzia mwezi Agosti, 2012. Kwa kuwarubuni watu kuwa viwanja hivyo ametumwa na
wafanyakazi wa CDA kuviuza.
Bw.
David Misime alitoa wito kwa wananchi wasikubali kurubuniwa kuwa wanauziwa
kiwanja na kutoa fedha bila kuthibitisha kiwanja hicho kama kipo na ni
halali.
CONTACT:
POLISI
MKOA WA DODOMA
DAWATI
LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
Phone:
0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi
(ASP)
Phone:
0712 360203, Silyvester Onesmo – Police
Konstebo (PC)
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
|
Post a Comment