Waziri Mkuu wa Mali Cheik Modibo Diarra ametangaza kujiuzulu wadhfa wake katika televisheni ya taifa, saa chache baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na wanajeshi wanaosadikiwa kuhusika na mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Cheik Modibo Diarra alikamatwa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Bamako, kwa kile kinachosemekana kuwa ni maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi hayo Kapteni Amadou Sanogo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Ufaransa.
Diarra alikamata madaraka ya Uwaziri Mkuu wa Serikali ya Mpito mwezi Aprili baada ya maafisa wa jeshi waliofanya mapinduzi kukabidhi madaraka mikononi mwa raia.