|
Kipa
Bara, Juma Kaseja (kushoto) akiokoa moja ya hatari mbele ya mshambuliaji wa
Zanzibar, Khamisi Mcha ‘Vialli’ katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa
michuano ya CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole Kampala
leo. Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika
120, Bara wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 10
kabla ya Abdallah Othman Ali kuisawazishia Zanzibar dakika ya
85.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars
inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, John Boko akiwatoka mabeki
wa timu ya Zanzibar Heroes wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika
michuano ya Cecafa Tusker
Challengeuliochezwa katika Uwanja
wa Nelson Mandela nchini Uganda
Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Haroub Nadir akimzuia
mshambuliaji wa trimu ya Zanzibar Heroes, John Boko wakati wa mchezo wa kutafuta
mshindi wa tatu uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini
Uganda.
Mchezaji wa timu ya
Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Athuman
Chuji akimtoka beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Sbari Alliy Makame wakati wa
mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Tusker Challenge
uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
|
on Saturday, December 8, 2012
Post a Comment