Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwenzi wa washindi
wa Amka Millionea, Ambapo moja kati ya washindi ni bw Rickson Richard kutoka
Arusha aliyejishindia shillingi million 15. pichani Katikati ni Meneja Bidhaa
Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw
Sadiki Elimsu.
Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami na
Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu wakitafuta
washindi wa mwenzi wa promosheni ya Amka Millionea ambapo Ambapo moja kati ya
washindi ni bw Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishinid kitita
cha shillingi million 15. wakishuhudia ni waandishi wa habari , kulia ni Afisa
Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde
akiongea na Mshindi wa Amka Millionea bw Rickson Richard (19) kutoka Arusha
mara baada ya kuibuka kuw mshindi wa shillingi million 15 wa promosheni ya Amka
millionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi
wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki
Elimsu
.............................................
Airtel
yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni
shilingi million 30
2 January
2013 Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo
iwatangaza washindi wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu
million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi
ambapo kila moja ameibuka na kitita cha shilingi milioni 15 pesa
taslimu.
Akitangaza
washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine
watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii
kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka
sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani
zaidi ya shilingi million 120. Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja
wa Airtel Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa
mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila
mmoja.
Tunaendelea
kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi
wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye
viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza
Matinde
Akiongea
kwanjia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi, Rickson Richard mkazi wa
Arusha na mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Lyamungo high school
alisema’ nimefurahi kuibuka mshindi wa milioni 15 wa promosheni ya Amka
millionea, pesa hizi ntazitumia katika masomo yangu shule na kumsaidia baba
yangu ambaye ndiye aliyenipa pesa za kuchezea promosheni hii. nawaambia
watanzania waamini wanaweza kushinda na kujiunga kwani
mimi nimecheza na nimeshinda kwa Bahati nao pia wananafasi ya kujishindia kama
mimi.
Tunapenda kuwajulisha kuwa promosheni hii bado
inaendelea na kukupa nafasi ya kuwa mmoja kati ya washindi wa mamilioni ya
fedha kila siku, kila wiki, kila mwezi au mshinid wa zawadi kubwa moja
itatolewa mwisho wa promosheni.
Ili mteja
aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure , Baada
kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo
atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila
ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na
kodi.
Post a Comment