Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo akihutubia kwenye uzinduzi wa Chanzo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo
akimwekea chanjo mmoja ya kati ya watoto walioshiriki kwenye Uzindu wa Chanjo
kwa Mtoto 13 Mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo
akishiriki kwenye buradani ya msanii mchelemchele muda mfupi baada ya Kuzindua
Chanjo kwa Mtoto 2013 Mkoani Mwanza Leo
---
Zoezi la Chanjo
limefanyika kimkoa katika Wilaya ya Sengerema kwenye Tarafa ya Sengerema
kijiji cha Sima na Kata ya Sima Mkoani Mwanza.
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evaristi Ndikilo amesema zoezi hilo kimkoa ni lazima lifanikiwe kwa mujibu wa
malengo walio jiwekea ya 95% kwa kila wilaya kinyume chake wale wote
watakaoshindwa kufikia lengo itabidi wajieleze na sababu zilizofanya washindwe
kuvuka malengo katika Mkoa wake.
Ndikilo amesema yeye kama mtendaji Mkuu katika Mkoa
wa wa Mwanza hayupo tayari kuona Mkoa huo unakuwa wa mwisho katika zoezi
hilo.
Amewahimiza wazazi kujitokeza kuhakikisha watoto wao
wanapatiwa chanjo hiyo kwani kuacha kuwachanja watoto, si hatari kwa mototo tu,
bali pia watoto wenzake wanao mzunguka hivyo ni vema kila mzazi akaona umuhimu
wakumpeleka watoto katika chanjo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa
Sengerema na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla wake kuwa, chanjo hiyo ni salama kwakuwa
imefanyiwa utafiti wakutosha na wataalam wa afya wa Ulimwenguni na Wizara ya
afya hapa nchini.
Akihututubia mamia ya wananchi wa kijiji hicho cha
Sima, Amesema watoto wa chini ya miaka 5 wanachangamoto nyingi, hasa kwenye
nchi zetu hizi zinazo endelea , kwani kwingineko kwa nchi zilizo endelea watoto
wanao zaliwa hukua kwa takriba ni 99% tofauti na hapa
kwetu.
Amesema ugonjwa wa kichomi huua watoto kwa 14%
ukitanguliwa na Malaria ambao huuwa kwa asilimia 15% huku ugonjwa wa kuharisha
ukishika nafasi ya tatu kwa kuuwa watoto wengi kwa asilimia 12% kwani nchini
Tanzania kila mwaka watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao takriba
ni 198,443 huugua ugonjwa wa kuharisha na kati yao 13,397 hufariki
dunia.
Ujumbe mahususi wa siku hiyo ni Jamii iliyochanjwa
ni Jamii yenye afya, ameongeza kuwa Chanjo hiyo ni sehemu ya Ilani, hivyo kufika
2015 jamii ya kitanzania iwe ni jamii iliyo na
ustawi.
Magonjwa ambayo hadi hivi sasa yana chanjo ni donda
koo, kichomi, kuharisha, pepopunda, kifua kikuu, surua, homa ya uti wa mgongo,
kifaduro, homa ya ini, na polio, haya ndio magonjwa yaliopo katika mpango wa
Taifa wa chanjo alisema na kuongweza.
Amehiza viongozi wa kila ngazi kuzindua kampeni
hiyo, na watoto walengwa ambao ni kuanzia wiki 6 hadi wiki 32 wapatiwe chanjo
hiyo bila kukosa.
Jumla ya watoto 149,000 wanategemewa kupatiwa chanjo
hiyo na amesema zoezi hilo ni endelevu hadi tarehe 31. DEC.
2013.
Post a Comment