Mwakilishi wa Kampuni ya
Kimataifa ya Mafuta na Gesi kutoka Nchini Ras Al Khaimah, Kamal Ahaya,
akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo VIP
Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Uongozi
wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi kutoka Nchini Ras Al Khaimah
ukiongozwa na Bwana Kamal Ahaya ukibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hatua za awali za kuanza kutekeleza
miradi saba ya Maendeleo na ustawi wa jamii Nchini.
*********************
Serikali ya
Ras Al Khaimah iko mbioni kutekeleza miradi saba iliyojipangia kuifanya hapa
Zanzibar katika harakati zake za Kusaidia miradi ya Kiuchumi, Maendeleo na
Ustawi wa Jamii wa Wananchi wa Zanzibar.
Maamuzi
yaliyofikiwa na Nchi hiyo kupitia Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na
Gesi Kutoka Nchini humo { CEO Rak Gas } ndani ya kipindi cha miezi miwili
iliyopita sasa yameanza hatua za utekelezaji.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi kutoka Nchini Ras Al Khaimah { Ceo Rak
Gas } Bwana Kamal Ahaya alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ukumbi wa Watu maarufu { VIP }
uliopo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Bwana Kamal
alisema uongozi wa Kampuni yake ambao upo Nchini kuanza hatua za utekelezaji wa
mpango huo unakusudia kutekeleza miradi saba miongoni mwake likiwemo suala la
Maji Safi, Ujenzi wa Hospitali moja kubwa ya kisasa pamoja na sekta ya
Elimu.
Mwakilishi
huyo wa Kamuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi ya Ras Al Khaimah alifahamkisha
kwamba miradi hiyo muhimu kwa ustawi wa Jamii itakwenda sambamba na wananchi
wenye mazingira magumu kuwezeshwa kujitegemea kupitia Taasisi inayosimamia michango ya
Nchi hiyo ya Al Rahma Charity.
“ Tumeamua
katika jitihada zetu za kusaidia Wananachi wa Zanzibar kuanza na ile miradi
muhimu zaidi katika jamii kama Afya, Elimu,Maji na kuwawezesha wananachi wenye
mazingira magumu Kimaisha”. Alifafanua Bwana Kamal
Ahaya.
Alielezea
faraja yake kutokana na mapokezi mazuri aliyoyapata yeye na ujumbe wake ambayo
yalimjengea mazingira muwafaka ya kuanza kukutana na washirika wakuu
watakaohusika na miradi hiyo hapa Zanzibar.
Kwa upande
wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru
Serikali ya Ras Al Khaimah kwa uwamuzi wake wa kutekeleza ahadi iliyotowa ambayo
imonyesha mwanga wa matumaini kwa wananachi walio wengi hapa
Nchini.
Balozi Seif
alisema miradi iliyopendekezwa na kupewa msukumo katika utekelezaj iwa mpango
huo itaweza kusaidia kupunguza au kuondosha kabisa matatizo yanayowasumbuwa
Wananchi hasa Afya na Maji safi na Salama miradi inayoendelea kutoa changamoto
kwa Jamii.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Ras Al Khaimah imekuwa mshirika wa karibu na
wa muda mrefu kwa Zanzibar katika jitihada za pamoja za kutafuta mbinu za
kutatua kero zinazowasumbnuwa Wananchi.
Mwakilishi
huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi Bwana Kamal aliwahi kukutana na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pia na
Mshauri wa Mkuu wa Mfalme wa Ras Al Khaimah Bwana Salem Ali Mwezi Novemba Mwaka
uliopita Mjini Dodoma.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/1/2013.




Post a Comment