Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi,
akifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Skuli Mpya ya Sekondari ya Mikindani
Dole Wilaya ya Magharibi, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za
kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi,
akimpongeza Mwakilishi wa Benki ya Dunia, anayeshughulikia Uchumi na
Elimu, Nobuyuki Tanaka, ambaye Taasisi
yake imegharamia ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Mikindani
Dole.
Bibi Tiba Vuai, akionekana mwenye furaha akipokea ufunguo wa chumba chake kutoka
kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika hafla ya
uzinduzi wa jengo lao lililofanyiwa matengenezo makubwa.
*********************
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kamwe haitakuwa na mjadala katika jukumu lake la kuendelea kuwatunza
wazee wasiojiweza wanaosihi katika makazi yao waliyotayarishiwa mara baada ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Kauli hiyo imetolewa na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizindua majengo
yaliyofanyia matengenezo makubwa pamoja na miundo mbinu katika makaazi ya wazee
yaliyopo Sebleni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema mchango wa wazee ni kubwa katika Taifa
hili hasa wakati wa harakati za kupigania
ukombozi wa Visiwa hivi jambo ambalo halina budi kutekelezwa na
kuenziwa.
Alisema suala la ujenzi wa
makaazi ya wazee wasiojiweza ni moja kati ya ahadi
zilizotolewa na Chana cha Afro Shirazy Party mara baada ya Mapinduzi na serikali
ya Mapainduzi ya Zanzibar inaandaa sera
Maalum ya
kuweka taratibu ya
kuwatunza wazee kisheria .
“ Utaratibu wa kuendelea
kuwatunza wazee upo kama kawaida kwani tunaelewa kwamba Jamii isiyo na utaratibu
huo inaeleweka kwamba imepotoka kabisa”. Alisisitiza Balozi
Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alitoa wito kwa mashirika ya Kitaifa na
Kimataifa zikiwemo Taasisi Binafsi kushirikiana na Serikali katika kuwatunza wazee
na kutoa rai kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu na Sekondari kutenga siku maalum ya
kujumuika na wazee katika harakati zao za usafi wa
mazingira.
Naye Waziri wa Ustawi wa
Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohd alisema
lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaondoshea aibu iliyokuwa
ikiwapata wazee wanaonyanyasika kutokana na ukosefu wa
makaazi.
Mapema Katibu Mkuu Wizara
ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Bibi Fatma Gharib
Bilal alisema ujenzi wa majengo hayo yaliyojumuisha nyumba moja, ukumbi wa
Mikutano, sambamba na miundo mbinu ya umeme na maji umegharimu zaidi ya Shilingi
MKilioni 429,900,000/-
Matengenezo hayo yamekuja
kufuatia kuungua kwa moto nyumba hiyo ya wazee usiku wa terehe 6/1/2011 ,ukosefu wa
uzio uliosabisha wizi wa vitu vyao na ubovu wa miundo mbinu ya maji na
umeme.
Katika mwishoni mwa
maendeleo ya shamra shamra za kutimia miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliifungua rasmi Skuli
mpya ya Sekondari ya Mikindani iliyopo Dole Wilaya ya
Magharibi.
Skuli hiyo mpya inatarajiwa
kuwaunganisha wanafunzi wa Skuli za Vijiji vya Dole, Kianga, Langoni,
Mwenge na Kijichi ikiwa na uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 320.
Zaidi ya shilingi Bilioni
Moja nukta Moja zilizotolewa mkopo na Benki ya Dunia zimetumika katika ujenzi wa
Skuli hiyo yenye majengo manne,Maabara, Maktaba ikiwa na wanafunzi 160 na walimu
16.
Akizungumza na Walimu
wanafuni na wananachi wa maeneo hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif alisema Serikali itaendelea kutafuta Walimu wenye sifa sambamba na Vifaa
ili kujenga Taifa bora lenye wataalamu wa
kutosha.
Balozi Seif alifahamisha
kwamba Taifa bado lina upungufu wa wataalamu, hivyo wanafunzi nchini wana nafasi
ya kuzitumia fursa zilizopo ambazo tayari serikali imeshawajengea mazingira bora
ya kielimu.
Mapema Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla Mzee alisema mradi wa
uimarishaji wa elimu ya lazima Zanzibar chini ya Mkopo wa Benki ya Dunia
umekusudia kujenga skuli 19 Zanzibar ambapo kila Wilaya itakuwa na Skuli mbili
za aina hiyo.
Nd. Abdulla alisema mradi
huo unaotarajwa kugharimu jumla ya dola za Kimarekani Milioni 42,000,000 sawa na
Shilingi Bilioni 62 za Kitanzania unahusisha pia uchapishaji wa
Vitabu.
Naye kwa upande wake
Mwakilishi wa shirika la Fedha Duniani {WB } katika masuala ya Elimu na Uchumi Bwana
Nobuyuki Tanaka ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua zake za
kuimarisha sekta ya elimu.
Bwana Tanaka alisema hatua
hiyo itaiwezesha Zanzibar kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka ya sayansi na
teknolojia ambayo tayari yanakamilika katika mfumo wa
Digital.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar
11/1/2013.
Post a Comment