SERIKALI
imesema imekuwa ikikerwa na utitiri wa vyama vya wafanyakazi nchini, ambapo
baadhi ya vyama hivyo vimekuwa vikianzishwa na wafanyakazi wachache kwa ajili ya
maslahi binafsi.
Kauli hiyo, imetolewa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, wakati akifungua semina ya elimu kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa sekta ya madini, iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) jana.
Alisema uwepo wa vyama vya wafanyakazi mahali pa kazi, ni utaratibu wa kisheria wa kimataifa ambao Tanzania imeridhia.
Lakini kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu wachache kuamua kuanzisha vyama vingine vya wafanyakazi vyenye malengo yale yale, mahali pa kazi kwa ajili kusaka vyeo kwa maslahi binafsi.
Alisema vyama, vinavyoanzishwa vimekuwa havina jipya na badala yake vimekuwa vikisababisha migogoro katika maeneo ya kazi na kuwafanya wafanyakazi kukosa vyama imara vya kuwasimamia katika mijadala mbalimbali dhidi ya Serikali.
“Serikali inapenda kuwepo na vyama imara vya wafanyakazi ili kuibana na kuhakikisha inatoa maslahi bora kwa wafanyakazi pamoja na waajiri wengine, leo hii STAMICO, inagawanyika na kuibuka kwa chama kingine cha wafanyakazi, lazima suala hili litazamwe upya ili kuondoa utitiri wa vyama vya wafanyakazi ambavyo vinawagawa,” alisema Waziri Kabaka.
Kuhusu suala la fao la kujitoa kwa wafanyakazi, Waziri Kabaka alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa kuwa Serikali inatarajia kuridhia kuwepo fao la kujitoa kuanzia Februari, mwaka huu na kueleza kuwa huo ni uongo.

CHANZO http://www.mtanzania.co.tz
Post a Comment