Chumba cha chini ya Bahari
kikionekana kwa mbali kikiendelea na matengenezo kwenye Hoteli ya Manta Resort
Makangale iliyoko Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akishusha Nanga kuashiria kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa chumba cha chini ya bahari katika Hotelai ya Manta Resort, iliyoko
Makangale Kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba jana.
Meneja wa Hoteli ya Manta
Resort Makangale mkoa wa kaskazini Pemba Bwana Metthew Saus {maarufu kama Babu
kwanini) na msaidizi wake wakiwa tayari kumsubiri mgeni
rasmi Balozi Seif Ali Iddi kuweka jiwe la Msingi na Nanga katika ujenzi wa
chumba cha chini ya bahari.
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif akiwa na Mkewe Mama Pili Seif
Iddi, wakiwa kwenye Boti kuelekea kwenye uwekaji wa jiwe la msingi na nanga ya
ujenzi wa chumba cha chini ya bahari katika Hoteli ya Manta Resort iliyoko
Makangale Mkoa Kaskazini Pemba.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mama Pili Seif Iddi akijigeza moja ya kanzu zilizotengenezwa na
wajasiri amali wa Jimbo la Gando ambayo aliondoka nayo kwa
manunuzi.
Balozi Seif akiwa na Mkewe
Mama Pili Seif Iddi wakifuaria bidhaa zilizotengenezwa wajasiri amali wa Jimbo
la Gando huku wakipata maelezo kutoka kwa mjasiri amali wa kikundi hicho Bibi
Faida Hamad Juma.
Wajasiri amali hao
walipata futrsa ya kutangaza bidhaa zao katika hafla ya uwekaji wa jiwe la nanga
la ujenzi wa chumba cha chini ya bahari hapo Manta Resort Makangale Kaskanzini
mwa kisiwa cha Pemba. Picha na Hassan
Issa wa – OMPR- ZNZ.
**********************************
Harakati za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sekta ya Utalii zimeanza kuonyesha
dalili za mafanikio kufuatia uwekezaji wa daraja la juu katika sekta hiyo kuanza
kushamiri kidogo kidogo hapa Nchini.
Ujenzi wa chumba cha
chini ya bahari { under water room} ulioanzishwa kama mradi maalum wa kuvutia
watalii wa daraja la kwanza unaofanywa na Uongozi wa Hoteli ya Manta Resort
iliyopo Makangale Mkoa wa Kaskazini Pemba ni miongoni mwa dalili
hizo.
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la
nanga la ujenzi wa chumba hicho kitakachokuwa chini ya Bahari ikiwa ni shamra
shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Balozi Seif akiambatana
na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Wizaraya ya Habari wakiwemo maafisa wa
sekta ya Utalii na wanasiasa alionekana kufarajika na mradi huo mpya ndani ya
Bara la Afrika na ni wa pili kufanywa Duniani ukitanguliwa na ule wa Sweden
ulioko katika maji ya ziwa.
Akizungumza katika hafla
hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema ni jambo la kutia
moyo kuona Kisiwa cha Pemba hivi sasa kinanza kupanuka Kiutalii kufuatia
kuimarika kwa miundombinu iliyowekwa.
Aliwataka wananchi wa
Kisiwa cha Pemba kuchangamkia sera ya Utalii kwa wote kwa lengo la kuitumia
fursa hiyo adhimu kabla haijavamiwa na wafanyakazi wa nje ya Visiwa
hivi.
‘’ Pemba sasa ni eneo
ambalo Serikali inaliangalia katika kufunguka kiutalii hasa kutokana na
kukamilika kwa miundombinu ya umeme na Bara bara’’. Alifafanua Balozi
Seif.
Alikumbusha kwamba
Zanzibar bado haijatangazwa kiutalii nje ya Nchi na watu wanaofikia hatua za
kufanya hivyo huitangazia kwa maslahi yao binafsi.
Balozi Seif ameiagiza
Taasisi inayosimamia uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA } kuziangalia upya
sheria zilizopo za uwekezaji ili kuwepuka kurejea makosa yaliyojitokeza tokea
kuimarishwa kwa sekta ya Utalii Nchini.
Alisema ipo miradi ya
uwekezaji ambayo imekuwa mtihani kwa serikali kwa vile imeshindwa kutoa huduma
zilizokusudiwa akiutolea mfano mradi wa Hoteli ya Mawimbini ambao kmwa sasa
umeshindwa kufanya kazi.
Akimkaribisha Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na
Michezo Mh. Said Ali Mbarouk alisema mradi huo wa chumba cha chini ya Bahari
masafa ya Mita 100 ni wa majaribio.
Mh. Said alieleza kuwa
mradi huo wa chumba kimoja utakapofaulu Uongozi wa
Hoteli ya Manta Resort umekusudia kujenga vyumba vingi zaidi ili kufanikisha
utali wa daraja la juu.
Mapema Meneja wa Hoteli
ya Manta Resort Makangale Bwana Metthew Saus Maarufu kwa jina la Babu kwa nini
alisema wazo la ujenzi wa mradi huu lilichukuwa takriban miaka saba kwa kufanywa
utafiti chini ya bahari.
Babu kwani alisema
Kisiwa cha Pemba kina mazingira mazuri ya kuendeleza mradi huo ikilinganishwa na
mradi wa mwanzo Duniani kama huo ulioanzishwa Nchini Sweden.
Amewapongeza wananchi wa
Zanzibar kwa kusherehekea miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964
yaliyowatoa katika makucha ya wakoloni.
Mradi
huo wa chumba cha chini ya Bahari unaokisiwa kugharimu Dola za Kimarekani Laki
Tano sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni Mia 758,000,000/- utakamilika rasmi
ndani ya muda wa siku Tisini.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar
8/1/2013.
Post a Comment