Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHADEMA KIMENUKA .... DKT SLAA AUMBULIWA KWA KUFANYA UFISADI WA KUTISHA NDANI YA CHADEMA. AKOMBA MILIONI 140 AMBAZO NI PESA ZA RUZUKU




HALI ya mambo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),si shwari baada ya kulipuka mgogoro mzito. Mgogoro huo, unamhusisha Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dk. Wilbrod Slaa kuwa amejikopesha mamilioni ya fedha ambazo hutolewa kama ruzuku kwa chama hicho, gazeti la Mtanzania limeandika.

Madai hayo yametolewa jana na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (BAVICHA), Juliana Shonza, alipokutana na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.

Katika madai yake, Shonza alimtupia alisema Dk. Slaa amejikopesha mamilioni ya fedha hizo, kwa matumizi yake binafsi.

Alisema tangu Dk. Slaa, alichukuwe mkopo hajawahi kurudisha jambo ambalo linazua masuali mengi kwa wanachama wa chama hicho.

“Nashangaa jambo hili kufumbiwa macho na Mwenyekiti wangu, Freeman Mbowe, fedha alizojikopesha Dk. Slaa ni za ruzuku ya Watanzania…nashangaa kuona fedha zote hizi zinashikiliwa na mtu mmoja, ukiuliza unaambiwa zimekwenda kwenye ujenzi wa chama mikoani, kama kweli tunataka kuingia Ikulu mwaka 2015, basi turekebishe mambo haya,” alisema Shonza.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kumshambulia kuwa tangu amefukuzwa amekuwa akitoa hoja za kitoto.

“Nasikitika kuona ananiambia natoa hoja za kitoto, nasema amenifedhehesha, ni dharau kwa vijana walioniona nina sifa na ukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti BAVICHA,

“Pili kauli yake, ni kama anahalalisha kikao batili kilichokiuka kanuni na Katiba ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yao yenye lengo la kuminya demokrasi na uhuru wa kujieleza ndani ya chama. Lakini pia anaonekana kuhalalisha hoja ambazo ndiyo uhalisia kuwa Heche hakuwa na sifa na uwezo wa kuchaguliwa katika nafasi yake, bali Mbowe ndiye alimbeba ili akae pale kwa malengo yake.

“Ndiyo maana, niliwahi kusema ukiona kifaranga cha kuku kiko juu ya figa, ujue mama yake yuko chini, kwa maana yake mama yake kifaranga kajitokeza kuhalalisha kupanda juu ya figa,” alisema Shonza.

“Mambo mengine, ambayo nimekuwa nikishauri ni matumizi mazuri ya fedha zinazokusanywa kwenye mkutano wa M4C na si kama zinavyotumika sasa, kitu kingine ambacho nimekuwa nikikipigia kelele ni hatua ya ndugu Slaa kujikopesha Sh 140 milioni ambazo ni fedha ya ruzuku ambapo hadi leo hajazilipa,” alisema Shonza.

Alisema kwa sababu kikao kilichomtoa si halali hadi leo hii, yeye ni Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA na kwamba taarifa zote zilizotolewa kuwa amevuliwa uanachama zipuuzwe.

“Nitaendelea kusonga mbele na nitadili na mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kunichafua kisiasa, nitadili naye iwe angani, chini ya jua na popote pale, sitamfumbia macho yeyote yule ambaye anataka kunichafua katika medani ya kisiasa,” alisema Shonza.

Wakati huo huo, Shonza alijikuta katika wakati mgumu, baada ya kuvamiwa na vijana watatu waliojitambulisha kama wanatoka CHADEMA makao makuu, wakimlazimisha kusaini na kupokea barua ya kuvuliwa uanachama wa chama hicho.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea kati ya saa 5 asubuhi katika hoteli ya Mic, iliyopo Ubungo, Dar es Salaam, ambapo watu watatu waliokuwa na gari yenye namba T 782 BPN waliwasili.

Watu hao, wakiongozwa na Ofisa Mwandamizi wa Usalama wa chama hicho, Hemed Sabula, waliingia ukumbini hapo kimyakimya, kisha kumfuata Shonza na kumtaka apokee barua yake, wakidai imetoka makao makuu ya chama.

Hali hiyo iliibua mtafaruku, baada ya Shonza kusema hamtambui mtu huyo na hana mamlaka ya kukambidhi barua ya kufukuzwa uanachama.

Hali hiyo iliibua mzozo ambapo Sabula aliendelea kumzonga Shonza na kutaka asaini barua hiyo.

“Chukua barua hii, umekuwa ukizunguka na kusema hujapewa barua toka umefukuzwa uanachama, barua yako hii hapa saini dispatch (kitabu cha kuonyesha barua imepokelewa), chukua ili uwaelezea sasa waandishi wa habari kwamba umepokea barua ya kufukuzwa,” alisema Sabula.

Kwa upande wake Shonza, ambaye alikuwa ameambatana na Mtela Mwampamba, aliyekuwa mgombea wa Ubunge Mbozi Mashariki mwaka 2010, ambaye naye amevuliwa uanachama, hawakukubali kupokea barua hizo.

DK. SLAA AGEUKA MBOGO

Baada ya tuhuma hizo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Slaa kupata ukweli wa madai hayo, lakini aligeuka mbogo na kujibu “nakwambia malalamiko haya siwezi kuyajibu, kwa sababu mimi ndiye mtu mwenye mamlaka ya rufaa, nasubiri niletewe mezani ndani ya siku 30.

“Lazima watu hao wafuate taratibu za chama, kama ambavyo tunaongozwa na Katiba… siwezi kubishana na mtu ambaye hafuati Katiba ya chama, kwani yeye alikuwa anazungumzia nini?” alihoji Dk. Slaa.

Alipoambiwa kuwa amemtuhumu kuchota kiasi hicho cha fedha, Dk. alikuja juu na kusema: “Sikiliza ndugu mwandishi, kama yeye alikuwa anazungumza mambo yake na akaamua kuongeza hayo mengine, mimi siwezi kuzungumzia hadi atakapokata hiyo rufaa yake na ukiandika vibaya tutakutana”.

HECHE NAYE JUU

Naye Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche, alipotafutwa kuzungumzia tuhuma, alisema: “Kama Shonza anaona ameonewa basi akate rufaa, anajua ni wapi, sisi ni chama ambacho kinafuata Katiba na si katika magazeti.

“Hizo tuhuma kwamba mimi ni kibaraka wa kiongozi fulani si kweli, akate rufaa, andika kama nilivyokwambia, kwa heri,” alisema John
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top