Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI KUFUATILIA MAENDELEO YA MIRADI INAYOZINDULIWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU

 

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu serikali kufuatiliaji maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge mjini Zanzbar.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.

Serikali inaandaa utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na kuwanufaisha wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na maendeleo ya miradi iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Amesema serikali ina wajibu wa kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2012 katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa gharama kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo inawanufaisha wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza hadhi na heshima ya Mwenge wa Uhuru.
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na kuongeza kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru unatumika tu kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa miradi hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top