MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji
(Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinayoonyesha kuwa petroli,
dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana
na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua
ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka
jana.
“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli,
dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa
lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta
ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa
hiyo.
Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli
katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya
taa Sh1,973. Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa
Sh2,057.
Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa
Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli
itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.
Taarifa
imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia
imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili
yaliyopita.
“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya
mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia
6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa
Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.
Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa
mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la
dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya
Marekani.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka
2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na
soko.
“Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa
kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la
kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,”
alisema Masebu.
Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo
wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa
bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo
kikomo.
Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo
mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo,
vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo
husika.
“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja
wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa
bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani.
Ni kosa kuuza mafuta bila
kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa
kituo husika,” alisema.
Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi
ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na
bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko
ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora
kisichofaa.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji
(Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinayoonyesha kuwa petroli,
dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.
“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli,
dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa
lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta
ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa
hiyo.
Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli
katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya
taa Sh1,973. Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa
Sh2,057.
Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa
Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli
itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.
Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.
Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.
“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya
mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia
6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa
Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.
Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa
mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la
dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya
Marekani.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka
2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na
soko.
“Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa
kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la
kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,”
alisema Masebu.
Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo
wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa
bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo
kikomo.
Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo
mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo,
vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo
husika.
“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja
wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa
bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani.
Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema.

Post a Comment