.
ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es
Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amelaani kitendo cha kupigwa risasi kwa
Padri wa kanisa hilo, Parokia ya Mpendaye mjini Zanzibar, Ambrose Mkenda na
kusema kitendo hicho hakileti matumaini mema kwa amani ya nchi katika siku za
usoni.
Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es
Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Desemba 24 mwaka 2012, Padri Mkenda alipigwa
risasi na watu wasiofahamika nje ya nyumba yake na kufikishwa katika Hospitali
ya Muhimbili ambako alitolewa risasi mbili.
Jana, Pengo akizungumza katika ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam, alisema tukio hilo na vurugu za kuchomwa makanisa ni ushahidi wa wazi kuwa watu hawaitaka amani nchini.
Jana, Pengo akizungumza katika ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es Salaam, alisema tukio hilo na vurugu za kuchomwa makanisa ni ushahidi wa wazi kuwa watu hawaitaka amani nchini.
“Padri wetu Zanzibar wakati anapigwa risasi
hakuwa anatoka kwenye vilabu vya pombe wala hakuwa katika majumba ya watu,
alikuwa anatoka kutimiza majukumu yake ya kiuchungaji lakini akapigwa risasi nje
ya nyumba yake, tunakwenda wapi?” alihoji Pengo.
Kadinali Pengo alisema vurugu za kidini zinazoendelea kujitokeza nchini hivi sasa hazileti dalili njema kwa amani ya nchi.
Kadinali Pengo alisema vurugu za kidini zinazoendelea kujitokeza nchini hivi sasa hazileti dalili njema kwa amani ya nchi.
“Hata hao wanaofikiri kuwa wakibaki pekee yao na
dini zao watakuwa salama hawapo sahihi kwani kuna nchi hivi sasa zipo katika
vurugu ingawa zina imani moja ya dini,” alisema Pengo.
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”
Alisema, “Angalieni nchi kama Tunisia, Algeria na nchi nyiingine hazipo salama ingawa zina imani moja ya dini.”
Alisema wanaochochea vurugu za kidini watambue
kuwa hata kama dini nyingine itaondoka na wao kubaki pekee yao hawatabaki
salama.
Kadinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa macho
na tofauti ambazo zinaweza kuleta vifo katika jamii kwani tofauti za kidini
zisiwe sababu ya kutukanana, kukashifiana kwani dini zote zinatoka kwa baba
mmoja hivyo haoni sababu za kujengeana chuki.
Pengo alisema mamlaka ya Serikali siyo kusimamia
msingi wa dini yoyote na inachaguliwa na watu wote hivyo kazi yake ni
kuwahakikishia watu wa dini zote usalama wao na mali zao na iwapo itashindwa na
kuwabagua watu kulingana na imani zao ni wazi kuwa itakuwa imepoteza
mwelekeo.
“Watu wa imani zote za dini wanapaswa kulindwa
na Watanzania wametakiwa kuliombea Taifa lao ili liweze kudumu katika imani na
mataifa mengine yaweze kuiga kutoka kwetu,” alisema Pengo na kuongeza kuwa Taifa
linahitaji maombi zaidi kipindi hiki kuliko wakati
mwingine.
Padri huyo alitolewa risasi mbili kinywani na
hali yake inaendelea vizuri na hadi juzi kulingana na taarifa za Jeshi la Polisi
Zanzibar, watu wawili walikuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kuhusiana na
shambulizi hilo na katika ghasia zilisababisha kuchomwa kwa makanisa Zanzibar na
Dar es Salaam watu kadhaa kesi zao zipo mahakamani
Post a Comment