Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FREEMASONS NA HEKA HEKA ZA MWISHO WA DUNIA - 2


 
Huu ni mwendelezo wa sehemu ya pili ya Heka heka zinazofanya na Freemason katika kuhakikisha Dunia inafikia Mwisho ikiwa ni sehemu ya kujitafutia ushindi kwa taasisi yao.
 
Kwa nini pawepo na mfululizo wa mijadala kati ya Al-Azhar University na Vatican; serikali ya Iran na Vatican na hata serikali ya Saud Arabia na Vatican?

Wiki jana nilielezea vyanzo vya baadhi ya makanisa. Sikuelezea historia ya kanisa la Roman Katoliki na lini lilianza.Lakini pia sikuelezea historia ya dini ya Kiislamu.

Kwa uchache kanisa la Roman Catholic ni kanisa la Roma, kama linavyojulikana, kanisa la Roma.Roma ni mji mashuhuri uliopo Italia. Mji wa Roma una historia ndefu katika dunia na ni mji uliotabiriwa na Mungu pia.

Dunia yetu imewahi kushuhudia ikitawaliwa na serikali moja katika awamu nne. Awamu ya kwanza ilikuwa ni serikali ya dunia iliyopewa jina la Babeli. Rais au mfalme wakwanza katika serikali hiyo alikuwa ni Nimrodi akifuatiwa na Nebukadneza pamoja na marais waliomfuata. Asili ya serikali hii ni mnara wa Babeli uliojengwa na mfalme wa kwanza wa Babeli, rais Nimrodi. Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali ya dunia awamu ya kwanza ni Iraqi.

Awamu ya pili ya serikali ya dunia iliitwa Mede/Uajemi ambapo mmoja wa marais wa serikali hii aliitwa Dario.Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali hii ni Iran ya leo. Awamu ya tatu ya serikali ya dunia iliitwa serikali ya Uyunani au Greece government. Mmoja wa marais mashuhuri katika serikali hii alikuwa ni Alexander mkuu (Alexander the Great). Awamu ya nne ya serikali ya dunia iliitwa ‘Roman Empire’ au himaya ya Roma. Mmoja wa marais wa serikali hii alikuwa ni Constantine. Serikali hii ndiyo iliyotawala kwa muda mrefu kuliko serikali zote zilizoitangulia.

Wakati serikali hizo zinatawala dunia, dini ya kweli ilikuwa haijatikiswa hadi serikali ya Roma ilipoanza kutawala. Je, dini ya freemasons ilianza lini? Ukiondoa dini aliyoianzisha Mungu katika bustani ya Edeni, dini ya freemasons ndiyo dini iliyoanza siku nyingi kuliko dini nyingine.Dini hii ilianzishwa pia kwenye bustani ya Eden mwanzilishi wake akiwa ni Shetani. Alimtumia Kaini anayejulikana kwa freemasons wa leo kama ‘first freemason’ yaani mjenzi huru wa kwanza.

Hatimaye rais Constantine kwa nusu aliamua kuachana na ibada za kipagani na kujiunga na Ukristo. Hii ilikuwa ni kutimizwa kwa andiko la 2 Wathesalonike 2:3,4 maana ulikuwa ni ukengeufu wa kanisa la mitume sehemu ya kwanza uliopelekea kuanzishwa kwa dini iliyochanganya ukweli na uongo. Kwa nini dini hii ilisubiri hadi awamu ya nne ya serikali ya dunia? Pengine nizungumzie kidogo maana ya namba nne kama inavyotumiwa na Mungu. Namba nne sio namba maalumu kwa freemasons lakini ni muhimu sana kwa Mungu. Namba nne inamaanisha kukomaa kwa mavuno na kuvunwa. Tazama hapa: “Akawaambia ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi…..Maana nchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena(pili)suke, kisha(tatu),ngano pevu katika suke. Hata (nne)matunda yakiiva mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika” Marko 4:26 – kwenye mabano ni ufafanuzi wa mwandishi. Hizo ni hatua nne kufika kuvunwa kwa mbegu njema. Vipi habari ya mbegu mbaya? “Lakini kila mmoja hujaribiwa(kwanza)kwatamaa yake mwenyewe. Halafuile tamaa ikisha kuchukua mimba(pili), huzaa dhambi (tatu), na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti(nne)” Yakobo 1:14,15. Unaweza pia kujua ni kwa nini waisraeli walitumia miaka 40 (4x10) kutoka Misri hadi Kanaani; kwa nini Yesu, Musa walifunga kwa siku 40 (4x10). Kumbuka kwamba namba 10 kwa Mungu inawakilisha ‘ukamilifu wa Mungu’ na namba 7 inawakilisha ‘utimilifu wa Mungu’.Kuna tofauti kati ya ‘ukamilifu’ – ‘perfection’ na ‘utimilifu’ – ‘fulness’.Kitu kinaweza kuwa ‘timilifu’ lakini kisiwe ‘kamilifu’ lakini kitu hakiwezi kuwa ‘kamilifu’ bila ya kuwa ‘timilifu’. Kwa mfano mapigo 7 ni utimilifu wa ghabu ya Mungu lakini ukamilifu wa hukumu yake utafikiwa wakati Shetani, dhambi na wadhambi watakapoangamizwa motoni. Mungu alitoa amri 10 kwa wanadamu ikimaanisha kwamba amri hizo zinawakilisha tabia ya Mungu ambayo ni ‘kamilifu’. Lakini pia tunasoma “….Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima na ‘ukamilifu’ wa uzuri” kisha anaanza kutaja ni kwa namna gani alikuwa ‘mkamilifu’ wa uzuri akisema “1)Akiki, 2)Yakuti manjano, 3)Almasi, 4)zabarajadi, 5)shohamu, 6)Yaspi, 7)yakuti samawi, 8)zumaridi, 9)baharamani na 10)dhahabu. Lusifa alikuwa ‘mkamilifu wa uzuri’ kutokana na kuvikwa aina 10 za madini ya thamani kubwa. Mungu ni‘mkamilifu’ kutokana na kuwa na tabia inayoelezewa kwenye amri 10katika Kutoka 20:4-17. Je wewe ni mkamilifu wa tabia kama ya Mungu kwa kuzitunza amri 10? Tafakari!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top