Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWANRI AKABIDHI VITABU



DSC00508Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akimkabidhi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri Vitabu vya Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa mara baada ya kuvizindua katika moja ya matukio ya shughuli zake za kikazi mkoani Rukwa. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Rutegwe.

………………………………………………………….
NA KIBADA KIBADA WA FULLSHANGWE-KATAVI

Watumishi wote wa umma wametakiwa kuwajibika vyema katika maeneo yao ya kazi na kila mmoja kwa nafasi yake katika utoaji wa huduma pale alipo ili kuleta maendeleo yanayokusudiwa kwa ujenzi wa Taifa.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano idara ya Maji Wilayani mpanda Mkoani Katavi mara baada ya kumaliza ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Wilaya ya Mlele Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri alihimiza uwajibikaji na utendaji kazi mzuri kwa kila mtumishi wa umma na kila mtu kwa nafasi yake katika jamii iwapo atatimiza wajibu ataweza kufanikisha suala la kuleta maendeleo kwa Taifa na yeye Mwenyewe.
Amesema uzalendo ni muhimu sana katika utendaji wa Kazi bila uzalendo katika kazi hakuna mafanikio, mataifa yote yaliyofanikiwa kiuchumi ni kutokana na uzalendo wa watu wake kuipenda nchi na kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa ili kufikia mafanikio waliyojiwekea.
Alisema watumishi wanatakiwa wachape kazi kwelikweli ili iwe mfano kwa wananchi wengine katika maeneo wanaokofanyia huduma ya utumishi wao,wajitume kwa nguvu zote.
Amesema serikali ina miundo mbinu mizuri sana iwapo wananchi wote wangekuwa na uzalendo wa kuisimamia kwa pamoja na kufanya kazi kwa nguvu kwa kujituma bila kusukumwa Taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo.
Katika ziara yake wilayani mpanda na Mlele ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa lengo la kuona fedha zinazoletwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama zinasimamiwa vizuri,na miradi iliyotekelezwa inalingana na thamani ya fedha yenyewe iliyotolewa na serikali kuu.
Akiwa wilayani Mpanda Naibu Waziri aliridhishwa na kiwango cha ,miradi aliyoitembelea na kuikagua ambapo alikagua mradi wa ghala katika kijiji cha Kibaoni,kisima cha maji kijiji cha Kilida, kituo cha habari za kilimo na soko la mazao Mwamapuli, miradi yote iliyoko wilaya ya Mlele ujenzi wa mnada Sibwesa na ujenzi wa daraja la Sibwesa lililoko Wilaya ya Mpanda.
Baada ya kutembelea miradi hiyo pia alifanya mikutano ya hadhara na kuwahutubia wananchi kuona umuhimu wa kutunza miradi iliyoko kwenye maeneo yao,kuwa ni mali yao pamoja na kutoa maelekezo kwa watendaji na viongozi kusimamia vizuri matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kuu kwa ajili ya maendeleo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top