IDADI ya
wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari
15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.
Hata
hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani
vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na
kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na
Zafarani Damoder.
Idadi
kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu
wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama
(Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus
Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na
Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James
Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida),
Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin
Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es
Salaam).
Naye
Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu
(TPL Board).
UCHAGUZI
TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika
Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru,
Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya
uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza
madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17
mwaka huu).
Mkoa
utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya
kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar
Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala
(Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Post a Comment