MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU NA WAKUU WA MIKOA WATOA MAONI KATIBA MPYA LEO
Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri leo katika
ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano uliolenga
kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Nyamrunda akiongea katika mkutano kati ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba
Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
leo.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa
Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
uliolenga kupata maoni ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu Katiba
Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yaokuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mawaziri Steven Wassira,
Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika na Prof. Sospeter Muhongo wakifuatilia mkutano
kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri
kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu
jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Angellah Kairuki akiongea katika mkutano kati ya Mawaziri, Manaibu
Mawaziri na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri
kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu
jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia akiongea katika mkutano uliofanyika katika
ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya.
Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abass Kandoro, Dkt. Rehema
Nchimbi (Dodoma) na Bi. Chiku Galawa (Tanga).
Wawakilishi wa Wakuu wa
Mikoa nchini wakipata maelezo kuhusu mfumo wa uhifadhi wa maoni ya wananchi
kuhusu Katiba Mpya yanayowasilshwa katika Tume kwa maandishi kutoka kwa Mjumbe
wa Sekretarieti ya Tume Bi. Flora Mkonya leo (Jumanne, Jan 15, 2013) katika
ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kanali (Mstaafu) Joseph
Simbakalia(Mtwara), Bw. Abass Kandoro (Mbeya), Bi. Chiku Galawa (Tanga).na Dkt.
Rehema Nchimbi (Dodoma).Wakuu hao wa mikoa pia waliwaslisha maoni ya Wakuu wa
Mikoa kuhusu Katiba Mpya.
Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Bi. Al-Shymaa Kway-Geer, Bw. Humphrey Polepole na Bi.
Riziki Mngwali wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Mawaziri uliolenga kupata
maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Post a Comment