Huu ndiyo ukumbi wa
Freemason uliopo Dar es Salaam.
Tangu miaka hiyo ya 1920 idadi ya vikundi vya Mason nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla imeendelea
kuongezeka. Ogezeko kama hilo hilo
limejidhihirisha katika Asia, Marekani ya
kusini, na baadaye Ulaya ya Mashariki, baada ya kipindi kile cha kuingia
kwa ukomanisti lakini kwingine kote hasa Ulaya ya Magharibi, Amerika ya Kusini na Australia, idadi ya Wanachama wa
Mason wamekuwa wakipungua polepole na kuacha pengo kubwa duniani kutoka milioni
saba waliokuweko wakati wa vita kuu ya kwanza hadi kufikia milioni tano
tu.
Hata hivyo mchango wanaodai kuutoa
ndugu hao millioni tano, kwa Chama chao na kwa Jamii, ni mkubwa sana. Wanatoa
misaada kila mwaka, kulingana na kazi zinazotekelezwa na vikundi vyao, kiasi cha
dola milioni 400 za Marekani. Huku Tanganyika, baadaye Tanzania, walisaidia
kituo cha watu wenye ukoma cha kindiwi wilayani Utete; Kituo cha watoto cha Mama
Theresa; shule ya Vipofu ya Pongwe,
mkoani Tanga; Kituo cha yatima cha Arusha, Hospitali ya Mnazi mmoja kula
Zanzibar; na Shule ya Viziwi ya Buguruni, ni machache tu kati ya miradi mingi
iliyogharimiwa na vikundi vya Mason.
Kati ya miradi hiyo yote, ule wa Shule
ya Buguruni ndio ninaouthamini sana moyoni mwangu; maana mimi ndiye mwandishi na
mchangishaji mkuu wa fedha; mhamasishaji na mtetezi mbele ya Viongozi Wakuu kwa
niaba ya shule hiyo kwa muda wa miaka thelathini iliyopita lakini bado pamoja na
shughuli zote hizo za maana, kwa muda wote huo niliokuwa Mwanachama wa Freemason
mara nyingi wale Wanachama wa Zamani wamenyanyaswa sana na magazeti ya nchi za Magharibi.
Kutoka kuonekana kuwa Chama ambacho
huruma na dhamiri zake katika kumwinua binadamu zinathaminiwa, kama ilivyokuwa
katika kipindi kirefu cha karne za kumi na nane na kumi na tisa na mwanzo wa
karne ya ishirini, sasa kimeporomoshwa hadhi kw amashambulizi makali ya magazeti
yasiyokuw ana msaada, kiasi cha kuigeuza Freemason kuwa kama kivuli tu, kikundi
cha wafitini cha ajabuajabu waliojaa hila!
Sir Andy Chande kulia akiwa na Rais Benjamin Mkapa |
Ili kuanza kukielewa vizuri zaidi
Chama hiki, na hivyo pengine kuanza kuoanisha dhana na hali halisi, lazima mtu
arudi kwenye misingi Freemason itikadi yenyewe ya Wema na maadili ndiyo
ilivyonitumbukiza katika mazungumzo yangu ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya 1950
na akina Campbell Ritchie na Maclean, juu ya huruma kwa binadamu. Wakati ule
ndipo nilipoanza kutambua kuwa, kumbe, maana kamili ya Uanachama wa Freemason ni
Sayansi ya Maisha ambayo lengo lake ni kumtia moyo mwanadamu kwa kumwelekeza vile anavyotarajiwa kuwa mtu
mwenye ukamilifu katika vyote.
Sehemu kubwa ya hoja hiyo ya Ukamilifu
wa mtu inafichwa katika dhana, na
pengine ndiyo maelezo ya uvumi unaoelekezwa kwenye shughuli za Freemason.
Lakini taratibu hizo zimejengwa kwa malengo ya makusudi, ambayo mimi nayaona
kuwa mazuri tu, ya kuamua na kuboresha fikra, moyo na hadhi ya binadamu kwa hiyo
katika hatua ya kwanza ya kuingizwa kwenye Freemason, mising mkuu ya maadili ya
kusema kweli inayojenga Freemason inasisitizwa kiasi cha kutosha katika mawazo
ya mtu anayetaka kujiunga na Chama au mtahiniwa.
Hatua ya pili ya Freemason inasisitiza
kuendelezwa kwa vipaji na ufundi katika sanaa na sayansi ili mtu aweze kuwa na
manufaa makubwa kadiri inavyowezekana katika maisha. Hatua ya tatu inatoa nafasi
kwa mtu kufikiria saa chache za mwisho wa maisha yake, lau kama hili litaonekana
kuwa kama ndoto kwa njia hivyo, huyo anayetaka kujiunga na Freemason anaelekezwa
namna ya kuishi kwa kutumia nafasi zote kabisa zilizopo katika namna inavyooana
na misingi mitatu ya Freemason, ambayo ni: Upendo wa kindugu, misaada na ukweli,
na kwamba kifo ni lazima.
Misingi ni mitatu ikisha kufafanuliwa
katika malekezo ya wakufunzi yanayositiri mengi kati ya matunda ya Freemason,
ndiyo ilivyovutia zaidi nilipopata kujua kwa ndani, kwa mara ya kwanza, baadhi
ya mambo katika kikosi cha Antient. Katika taratibu za Freemason, mzingi wa
upendo wa kindugu unawaelekeza ndugu zetu wote kuwatambua binadamu wote kuwa familia moja iliyoumbwa na
huyo Mwenyezi, lakini wakati huo “msaada” unatoa ujumbe kuelekeza imani
niliyofunzwa na baba yangu, yaani kuwasaidia
wenye shida iwe katika kuwapunguzia umasikini, au kuwaliwaza
wanaosumbuliwa na matatizo. Huo ni wajibu wetu sisi sote.
“Ukweli”, msingi wa tatu nap engine,
ndio muhimu kuliko yote ni dhana takatifu ambayo, kwa mwanachama wa Freemason,
ndio msingi wa kila jema la binadamu “kuwa mtu mwema na kweli” ni somo
linalotolewa mapema kwa kila mtu anayetaka kuingia katika Freemason; hivyo ni
kauli inayotumiwa kila mahali kama zana ya kurekebisha na, kama ikibidi
kuelekeza njia ya maisha na vitendo vya mtu kulingana na masharti yale manne
muhimu ya Freemason: kiasi, uvumilivu, busara na haki.
Na misingi yote hii, na maadili na
umuhimu unaojumuisha siyo tu mafunzo ya falsafa za watu wa kale, kuanzia
wagiriki, paka Budha, mpaka Zaroster. Lakini hata za dini zinazojulikana.
Kinyume na propaganda zinazoenezwa za Mafashisti wa kiitaliano na wengine wengi
zaidi ya hao, Freemason si chombo cha
dini wala vile vile, kinyume chake, hakipingi dini; kwa kweli Freemason
wanawakaribisha watu wote bila kujali imani zao za dini, wala hawafanyi mbinu za
kubadili imani zao wala kuelekeza ibada zao; wanachojaribu tu ni kuwafanya
binadamu bora zaidi.
Sir Andy Chande akiwa na wenzake wakipanda Miti jijini Tanga kama moja ya shughuli zao za kijamii |
Hivyo hiyo ndiyo dunia niliyoitumbukia
mwaka 1954, na ikawa sehemu muhimu ya maisha yangu kuanzia hapo. Katika kipindi
hicho nimepata bahati ya kushuhudia kujitolea kwa Wanachama wa Freemason katika
kuwasaidia wenye shida ndani ya Afrika Mashariki na hata nje ya hapo. Nimepata
kutambua umuhimu wa mafunzo ya Freemason katika kujenga hisia za utuwema na
ukweli kwake mtu wenyewe na kw abinadamu wenzake. Moyo wangu mawazo yangu na
roho yangu, vyote vimeimarika kutokana na kushiriki kwangu katika Freemason; na
kuimarika huko kunatofautiana kabisa na hisia zinazotangazwa katika magazeti
mashuhuri ya nchi za magaribi. Kuwasaidia wenzetu kuwasaidia wengine ndiyo
misingi niliyojifunza katika miaka yangu mingi ndani ya Freemason.
Baada ya kushika nafasi za juu zaidi
katika kambi hii ya Nyota ya Jaha mnamo miaka ya mwisho wa 1950 na 1960
nikateuliwa kuwa kiongozi mstahiki mwaka 1967, wakati huo ndio kwanza
nimeteuliwa Rais wa Muungano wa vyama vya Round Table vya Afrika Mashariki. Mwaka uliofuata, kwa vile
nilivyokuwa Mwanachama wa kwanza wa Round Table asiyekuwa Mzungu, nikawa raisi
wa kwanza wa Roundi Table na vyama vinavyoambatana nayo duniani mwenye asili
isiyokuwa ya kizungu: ukweli ulioinua hadhi ya nafasi hii kwa kiwango kikubwa
zaidi kuliko ilivyokuwa
kawaida.
Kwa nafasi hiyo nikalazimika kusafiri
sana, kuandamwa na Magazeti, na kuwa na shughuli nyingi za uwakilishaji
kimataifa, mwaka 1970 nikakamilisha kipindi changu cha uongozi kama rais wa
Kimataifa wa Baraza la Dunia la Klabu ya Huduma za Vijana; na mwaka uliofuata,
baada ya kulazimika kustaafu kutoka katika chombo hicho kwa sababu ya umri,
nikiwa makamu wa kudumu (wa heshima) wa Mwenyekiti wa Muungano wa Round Table
katika Afrika Mashariki mwaka 1970 nikajiunga na Round Table ya Dar es salaam,
hatua ya kwanza kuelekea kwenye nafasi ya Gavana aliyewajibika na klabu sabini
na nane katika sehemu kubwa ya Afrika.
Mwaka 1972 nikachukua hatua yangu ya
kwanza kuelekea kwenye madaraka makubwa zaidi katika Freemason nilipochaguliwa
Afrisa Mkuu wa Wilaya wa kufanya kazi na Makao makuu ya Freemason ya Mkoa kule
Nairobi ambao wakati ule ulikuwa unasimamia makambi kiasi cha ishirini na manane
katika Afrika nzima.
Kila nilivyopata madaraka makubwa
zaidi, ndivyo nilvyohakikisha kwamba nilifanya kila lililowezekana kutakasa
Freemason mbele ya Umma. Kwa uzoefu wangu mimi, watu kwa kawaida hutilia
mashaka, na hata kuogopa, mambo wasiyoyaelewa. Kwa hiyo wakati wote nilipoulizwa
habari za Freemason nikajitahidi kumweleza huyo muulizaji misingi ya chombo
hicyo, nikisisitiza kwamba hakikuwa chama cha siri, na wanachama wake
wanajulikana wazi: na kwamba mikutano yake haifanyiki katika sehemu za kujificha
ila katika kumbi za mikutano zinazojulikana, zenye hati ya serikali na
zinazoweza kutambulika wazi wazi.
Kama nilivyokwisha kusema mapema chama
hiki na maajabu yake, kiliingia wakati wa Vita Vikuu vya pili, tulipokuwa
tunajaribu kuwalinda wanachama wetu waliokuwa Italia, ufaransa na Ujerumani
dhidi ya vituko vya mataifa makubwa toka wakati huo tumejidhihirisha wazi wazi
mbele ya umma, na kujitahidi wakati wote kuwaondolea mashaka na kudhihirisha
kuwa chama chetu ni chombo kinachomwingiza mtu mwema na kujitahidi kumfanya
mwema zaidi.Habari yote hii ni kwa Mujibu wa kitabu cha Sir Andy
Chande
Source:Jibu la Maisha Jamii
Forum
Post a Comment