Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JK AONGOZA CHA ASASI YA SIASA,ULINZI NA USALAMA CHA SADC ,RAIS ANDRY RAJOELINA WA MADAGASCAR NA KUFIKIA MAKUBALIANO MAALUM

 



NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAKUU wa nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuia ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika(SADC TROIKA) wamekubaliana kusaidiana na umoja wa Mataifa(UN) wa kupeleka Majeshi ya Ulinzi na Usalama(NIF) katika upande wa Mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo(DRC) .

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC), Tomaz Salomao wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wakuu hao uliofanyika kwa muda wa siku mbili jijini Dares Salaam.
Mkutano huo ulimalizika leo ambao ulikuwa unajadili hali ya siasa na usalama kwa nchi za DRC, Zimbambwe na Madagascar chini ya Mwenyekiti wake (SADC TROIKA) Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Rais wa Namibia, Hifikepunye Pohamba, Rais wa Msumbiji , Armando Emilio Guebuza, ambaye ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Msumbiji , Jacob Zuma .
Akizungumzia kuhusu upande wa DRC Salomao alisema “mkutano huo umetaka misaada ya kibinadamu ipelekwe mapema iwezekanavyo katika upande wa Mashariki mwa DRC.
Salomao aliongeza kuwa wamepokea ahadi za nchi za Malawi, Namibia, Afrika Kusini na Tanzania za kuwa tayari kupeleka majeshi ya ulinzi na usalama katika upande huo , ambapo pia umezishauri nchi nyingine ambazo hazijatoa ahadi hizo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Akijibu swali la mwandishi wa habari kuwa kila nchi itachangia wanajeshi wangapi na lini watakwenda Rais Kikwete alisema suala hilo bado liko kwenye mchakato.
Kwa upande wa Zimbabwe Salomao alisema mkutano huo umependekeza wadau wa siasa katika nchi hiyo kuhakikisha wanaharakisha wanakamilisha utengenezaji wa Katiba mpya ili kuwezesha uchaguzi wa amani, huru, na haki .
Aliongeza kuwa katika mgogoro wa kikatiba wa nchi ya Madagascar mkutano huo umepokea maelezo, kutoka kwa Rais wa mpito wa nchi hiyo ,Andry Rajoelina kuhusu mkakati wa kutatua suala hilo na kusisitiza utekelezaji wake.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top