Hawa ni waigizaji katika tasnia ya maigizo na filamu hapa nchini.Walikutana katika filamu ya mboni yangu na kuwa wapenzi.Katika mapenzi yao walivalishana pete za uchumba na hatimae kupanga kufunga ndoa.Siku chache kabla ya ndoa yao walipata ajali na Wastara kuvunjika kabisa mguu.
Watu wakajiuliza kweli Sajuki atamuoa Wastara pamoja na kukatwa kabisa mguu?Baada ya wastara kupona jeraha ndoa yao ikafungwa dada akitembea kwa magongo.Baadae alifanikiwa kupata mguu wa bandia na sasa anatembelea mguu wa bandia.
Mitihani haikuishia hapo katika familia hii ambayo wamejaaliwa mtoto
Baada ya kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.
Mwezi wa kumi na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la kuwashukuru watanzania walipomchangia.Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.Akiwa mkoani Arusha
katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema
“Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”
Baadae mwenyewe alisema kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine. na muda wa kurudi ulikuwa umefika.
Kwa takribani wiki mbili Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.Na ilifikia hatua ya mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kumsaidia kumpeleka India kwa matibabu.
Post a Comment