Waombolezaji wa Msiba wa
Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza
lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa
Marehemu Tabata Bima.Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk
Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili
utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye
gari.
Dua ikisomwa kabla ya
kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma
Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani
mapema asubuhi hii.
Pamoja na kwamba kulikuwa
na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili
ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye
Mazishi.
Mwili ukiondoka
nyumbani.
chanzo: Father Kidevu
chanzo: Father Kidevu
1 comments:
KUKOPY SIO DHAMBI LAKINI ANDIKA HABARI HIYO UMEITOA WAPI SIO VIZZURI NA MUWE NA HESHIMA YA KAZI ZA WENZENU.........................
ReplyPost a Comment