Bondia wa ngumi za kulipwa na
bingwa wa IBF INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda
ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la
kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa D.I.D Hall uliopo mabibo
mwasho.
Mratibu wa pambano hilo Charles
Christopher mzazi ameeleza kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na
mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani na wamepima wapo sawa
kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya
utangulizi na mabondia watakaosindikiza pia wamepima chini ya usimamizi
wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa
kupambana.
Mabondia watakaocheza utangulizi
ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI
atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO
MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na
JUMA J KASHNDE.
Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa
nchini Ibrahim Kamwe ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu
za ngumi za kulipwa zimefuatwa na mabondia wapo katika hali nzuri ya
kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi wa DID HALL mabibo mwisho
kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI SHAURI na SAID
NJECHELE


Post a Comment