Maxmilian
Bushoke akiwa na mtoto wake Bushoke nyuma.
Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI
wa siku nyingi nchini, Maxmilian Bushoke, anatarajia kutambulishwa rasmi katika
kikosi cha wanamuziki wa bendi ya Orchestra Mlimani Park, baada ya kurejea
nchini hivi karibuni na kujiunga na bendi hiyo.
Bushoke
alikuwa akiimbia bendi hiyo tangu miaka ya kati ya 1980, kabla ya kuhamia nchini
Afrika Kusini alikokuwa akifanya shughuli za utangazaji.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa
bendi hiyo, Jimmy Chika, alisema Bushoke atatambulishwa katika Ukumbi wa
Pentagon, uliopo Kurasini ambapo pia atafanya shoo na wanamuziki wenzake kuanzia
Jumapili ya Januari 20.
Mwimbaji
huyo na mtunzi aliwahi kujizolea sifa baada ya kutunga nyimbo kama Kiu ya Jibu,
Penzi kile cha fikara na nyingine kadhaa.
Bushoke
ambaye ni baba mzazi wa msanii wa kizazi kipya, Luta Bushoke, amekuwa akijiunga
na bendi hiyo mara kwa mara alipokuwa akirejea hapa nchini, ambapo hata hivyo
sasa atakuwa na bendi hiyo kwa kipindi kirefu.



Post a Comment