![]() |
| Mfungaji
wa bao la Azam leo, Samih Hajji Nuhu akipongezwa na Mwaikimba |
AZAM FC imeanza vibaya
ziara yake ya Kenya, baada ya kufungwa mabao 2-1 kwa tabu na wenyeji AFC Leopard
katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, jioni
hii.
Mabao ya washindi katika
mchezo huo, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la Azam lilifungwa na
Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
Hata hivyo, Azam itabidi
wajilaumu wenyewe kupoteza mchezo huo, kwani walipoteza penalti mbili kupitia
kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Pamoja na kufungwa, Azam
ilionyesha soka maridadi jioni ya leo mjini hapa kiasi cha kuwavutia mashabiki
wa Kenya, waliojikuta wakiishangilia baada ya kuzimikia soka
yao.
Katika mchezo huo, kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, Luckson
Kakolaki, Joackins Atudo, Abdulhalim Humud/Ibrahim Mwaipopo, Jabir
Aiziz/Humphrey Mieno, Salum Abubakar/Kipre Balou, Gaudence Mwaikimba/Brian
Umony, Khamis Mcha na Uhuru Suleiman/Abdi Kassim
‘Babbi’.



Post a Comment