Kikosi cha
Yanga
Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
MABINGWA wa zamani wa
Tanzania Bara, Yanga SC, leo imewaangushia kipigo cha mbwa mwizi wageni wao,
timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, baada ya kuwatandika mabao
3-2.
Mabao ya Yanga
yalipatikana katika dakika ya 32 lililowekwa kimiani kwa njia ya penati na
Jerryson Tegete, Frank Domayo dakika ya 63, kabla ya 72 Tegete alipoongeza
kalamu ya mabao kwa kuandika bao la tatu.
Mabao ya Black Leopards
yalipatikana katika dakika ya 46 lililofungwa na Hampherey Khoza, huku lile la
pili likifungwa na Rodney Ramagaleki katika dakika ya 88, hivyo matokeo kuwa bao
3-2.
Mchezo huo ulikuwa na
ushindani wa aina yake, kutokana na timu zote mbili kukamiana kwa ajili ya
kuipatia ushindi, ila Yanga wao walikuwa juu zaidi na kufanikiwa kuibuka na
ushindi huo mnono.
Mchezo huo ni wa
Kimataifa wa kirafiki uliowakutani katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
ukiwa ni mchezo mahususi kwa ajili ya kuwapima wachezaji wa Jangwani waliokuwa
kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.
Pia mchezo huo ni sehemu
ya maandalizi kwa timu ya Yanga inayojiandaa na mzunguuko wa pili wa Ligi ya
Tanzania Bara, huku wao wakiwa kileleni.
PICHA ZAIDI ZA MECHI HIYO .....
Yanga 3-2 Black
Leopard

Golikipa wa timu ya Black
Leopards,Ayanda Mtshali akijaribu kuokoa mpira uliotinga kimiani kwa njia ya
penati na mchezaji wa yanga,Jerson Tegete,penati hiyo ilipatikana katika kipindi
cha kwanza,katika kuoenesha Yanga wako fiti mnamo kipindi cha pili mchezaji
akaongeza goli la pili,haikutosha Tegete tena akapachika goli la 3.Ihii ndiyo
Yangaa.
Mchezaji wa timu ya
Yanga,Mbuyu Twite akimtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini.Ama kwa hakika ihiiii ndiyo Yanga ya Uturuki iliotandaza kabumbu safi
kabisa ndani ya Uwanja wa Taifa.
Mchezaji wa timu ya
Yanga,Frank Domayo akitaka kumtoka mchezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini,kwenye mchezo wao wa kirafiki unaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa hivi
sasa.
Baadhi ya mashabiki
wakifuatilia mtanange wa Yanga na timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini.
Mashabiki wa yanga
kibao
Full Nginja
ngijaaa
Mashabiki kwa shangwe kila
wakati wakiipa hamasa ya ushindi timu yao ya Yanga.
Mchezaji wa timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini akitaka kuwapangua wachezaji wa timu ya Yanga,aah
iwapi kwa taabu sana kama uonavyo pichani.
Baadhi ya wachezaji wa
Black Leopards ya Afrika Kusini wakiwa kwenye benchi lao
Baadhi ya makocha wa yanga
na wachezaji wakiwa watulia tulii kwenye benchi lao la Ufundi
Sehemu ya kikosi kazi cha
Clouds TV kinachorusha mtanange huo live kupitia Clouds TV jioni ya
leo
Wachezaji wa timu ya Yanga
wakiingia iwanja kuiana ngwe ya kwanza.
Hiki ndiyo kikosi kazi cha
Yanga
Kikosi cha Black Leopards
ya Afrika Kusini.
Post a Comment