Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Ali Juma Shamhuna mara alipowasili katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya
Kaskazini “A”kwa ajili ya kufungua Skuli ya Primary yenye madarasa Manne,ikiwa
ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad akikata Utepe kuashiria kufungua Skuli yenye madarasa manne katika Kijiji
cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya
Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad akipanda Mche wa Mnazi baada ya kuupanda katika eneo la Skuli ya Mbuyu
Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,Baada ya Kuifungua Skuli hiyo ikiwa ni Shamra
shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu
Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,wakifurahia Baada ya kufunguliwa kwa Skuli yao
ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewataka Wazazi na Walezi wa
Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende kujenga Mashirikiano na Walimu ili kuweza
kuwapatia haki na fursa sawa wanafunzi wa kike na wakiume Skulini hapo.
Hayo ameyasema leo huko Skuli ya Msingi Mbuyu
Tende Wilaya Kaskazini “A” Unguja wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni
mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Maalim Seif amewataka Wazazi wasikubali
kuwaozesha watoto wa kike waume mapema kwani hali hiyo ndiyo inayochangia
ukosefu wa Walimu wa kike wazawa katika Vijiji
vingi.
Aidha alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
inaendelea kuwapatia wananchi wake haki ya elimu bila ya malipo ili kuondosha
adui ujinga na kuwaletea maendeleo.
“Elimu ni msingi wa maisha kwa vijana na ndio
inayoleta maendeleo na mwangaza hasa wakati wa sasa na ujinga ni kiza katika
maisha ya leo,”alisisitiza Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar.
Alisema kuwa wanafunzi wakipata msingi mzuri wa elimu
wataweza kupambana na mazingira ya sasa ya sayansi na teknolojia kwa kwa ufanisi
mkubwa.
“Tusitazamie vijana kupata maisha mazuri bila ya elimu
hasa katika zama hizo za sayansi na tecnologĂa kwani elimu ndio kila
kitu’’alisema Makamo wa Kwanza .
Maalim Seif aliitaka Idara ya Mitaala kuandaa mbinu
bora za ufundishaji wa mafunzo ya amali ili wanafunzi wakimaliza masomo yao
waweze kujiajiri wenyewe na kuweza kuondosha mzigo kwa
Serikali.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Ali Juma Shamhuna alisisitiza wananchi wa kijiji hicho kuchukua juhudi ya
kuwasimamia watoto wao hasa wa kike kupata elimu kwani wanauwezo wa kufanya
vizuri zaidi katika masomo.
Aidha katika uzinduzi huo zaidi ya shilingi milioni 11
zilichangwa kwa ajili ya maendeleo ya skuli hiyo ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais
alichangia milioni tano na Waziri Shamhuna milioni tatu.
Ujenzi wa Skuli ya Mbuyu Tende umegharimu jumla
ya shiling Milioni 44 kwa ajili ya kujengea jengo lenye madarasa manne pamoja na
kununua madawati kwa Skuli hiyo.
Post a Comment