Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa,
iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa hafla ya uzinduzi huo
iliyofanyika leo, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary
Yusuph Mzee, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Hoteli hiyo, Alexandro
Azola.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka
kwa mhudumu wa mapokezi wa chumba cha mazoezi na masaji, Zuhura Saleh (kushoto)
wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na mazingira ya Hoteli ya ya Kitalii
ya Gold Zanzibar Beach House & Spa, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja,
wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo, uliofanyika leo, mjini Unguja. Kulia
ni Waziri wa Fedha, Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee.
Moja ya sehemu ya Mandhari
ya Hoteli hiyo........
Mkurugenzi wa Hoteli hiyo
akimuonyesha Makamu moja ya Chumba cha Hoteli hiyo......
Sehemu ya Bwawa la kuogele
'Swimming Pool'......
Sehemu ya Hoteli hoyo ya
Nyota 5, inavyoonekana mbele yake kukiwa na 'Swimming
Pool'.....
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Zanzibar Beach House & Spa,
Alexandro Azola (ushoto) wakati alipokuwa akitembelea kukagua maeneo na
mazingira ya Hoteli ya hiyo, iliyopo Mkoa wa Kaskazini A, Unguja, wakati wa
hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo, mjini Unguja. Kulia ni Waziri wa Fedha,
Zanzibar, Mhe. Omary Yusuph Mzee.
Makamu na ujumbe wake
wakiondoka katika eneo hilo la Hoteli baada ya uzinduzi.
Post a Comment