Kamanda wa Brigedia nyuki Brigedia General Sharif
Sheikh, akiwa pamoja na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif,
wakifurahia mwenendo mzima wa matayarisho ya gwaride la Vikosi vya Ulinzi yaliyokuwa yakifanyika katika
uwanja wa amani MJINI Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni
mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya sherehe na mapambo Balozi seif, akiwa na Waziri
wake Kulia Mh. Mohd Aboud Mohd na Kamanda wa Brigedia Nyuki Brigedia General
Shjarif Sheikh wakiangalia matayarisho ya mkwisho ya gwaride la sherehe za
mapinduzi katika uwanja wa amani Mjini Zanzibar.
'Watoto wa Kazi' Kikosi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa
Tanzania { JWTZ }, Kikionyesha umahiri wake ndani ya Uwanja wa amani wakijiandaa
na sherehe za maapinduzi zinazofanyika kesho Jumamosi Tarehe 12 Januri 2013,
katika uwanja huo.
Msanii wa Kikundi cha Utamaduni cha Hiari ya Moyo
kutoka Mkoani Domoma kikipasha moto kujiandaa na utoaji burdani kwenye sherehe
za maaadhimisho ya kutimia miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar zitakazofikia
kilele chake januari 12 2013.
Kikundi cha Utamaduni ya
mchanga mdogo kisiwani Pemba kikitoa burdani ya ngoma ya msewe katika
matayarisho ya maadhimisho ya sherehe za kutimia Mikaka 49 ya Mapinduzi ya
Zanzibar hapo Uwanja wa Amani.
***************************
Wakati harakati za shamra
shamra za maadhimisho ya kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya
Mwaka 1964 zikikaribia kufikia kileleni matayarisho ya mwisho ya gwaride la
kuhitimisha sherehe hizo zimekamilika
rasmi.
Matayarisho ya Gwaride hilo ambalo
ndilo linalopamba maadhimisho ya sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar
yamefanyika katika uwanja wa Amani Mjini
Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Taifa ya sherehe na Mapambo ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi akiwa na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Baadhi ya maafisa
wa Vikosi vya ulinzi walishuhudia matayarisho
hayo.
Vikosi vya ulinzi vya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania { JWTZ } Polisi, KMKM, Mafunzo, JKU, Valantia na
Zimamoto na uokozi vilianikiza ndani ya uwanja wa Amani wakati vilipokuwa vikitoa
burdani ya gwaride la aina yake vikiongozwa na Vikosi vya
Bendi.
Wakipita mbele ya
mwenyekiti huyo wa Sherehe na Mapambo Balozi Seif Askari hao walionekana kuwa
katika hali ya ukakamavu baada ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa kipindi cha
mwezi Mmoja.
Staili ya mwendo wa pole na
ule wa haraka zikimalizia kwa heshima mbele ya Viongozi hao ilionekana
kukubalika vyema na walioshuhudia matayarisho hayo kutokana na makofi ya
vigeregere wakati wakitoa heshima zao.
Raha zaidi ilionekana
kuwakonga moyo walioshuhudia zoezi hilo wakati maafandi hao walipomalizia kwa
hatua 15 zilizofuatiwa na ule wimbo maarufu unaomuhusu kila mwanafunzi anayepata
elimu ya dunia katika maskuli wa sisi sote
tumegomboka.
Matayarisho hayo
yalifuatiwa na burdani za vikundi vya utamaduni vya Msewe kutoka Mchanga mdogo
Kisiwani Pemba, Mkunguru kutoka Kaskazini Unguja na Hiari ya Moyo kutoka Mkoa wa
Dodoma Tanzania Bara sambamba na Vijana wa halaiki kutoka Skuli ya Sekondari ya
Nyerere.
Akizungumza na Wajumbe wa
Kamati ya Taifa ya Sherehe Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa matayarisho ya
Gwaride hilo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Seif Ali Iddi amewashukuru na
kuwapongeza Makamanda na askari wa vikosi vya ulinzi kwa juhudi zao za
matayarisho makini.
Balozi Seif alielezea
matumaini yake kutokana na matayarisho hayo kwamba sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar kutimia Miaka 49 mwaka huu zitakuwa nzuri na za aina
yake.
Wakichangia kwenye kikao
hicho cha mwisho baadhi ya wajumbe wa Kamati hayo wamewaomba wanachi
watakaobahatia kuingia katika uwanja wa sherehe waache kuchukuwa mikoba ambayo
inaweza kuwaletea usumbufu wakati wanapotaka kuingia uwanjani
hapo.
Hata hivyo wajumbe hao
wamependekeza kwamba kikundi au taasisi itakayopangwa kwa tukio lolote kiwanjani
hapo wakati wa sherehe hizo wakazingatia zaidi wakati ili kwenda vizuri na
ratiba iliyopangwa.
Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar
11/1/2013.

Post a Comment