Jeshi la polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam inawashikilia askari polisi watano kwa tuhuma za upotevu wa
fedha kiasi cha shilingi milioni 150 mara baada ya tukio la uporaji
lililofanyika eneo la Kariakoo mnamo tarehe 14/12/2012.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Polisi Dar
es Salaam Suleiman Kova (pichani) amesema baada ya tukio hilo zilipatikana
taarifa kuwa fedha hizo zilipotea baada ya mtuhumiwa Augustino Kayula na Frank
John Mwangiba kukamatwa akiwa na bastola aina ya Browing lakini hakuwa na fedha
zilizoporwa, na ambaye anasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na
wenzake.
Kamanda Kova amesema pamoja
na kukamatwa kwa askari hao pia wamekamatwa majambazi wawili waliohusika na
tukio hilo ambao ni ambao ni Deogratias Kimaro mkazi wa Kilakala na Kulwa
Mwakabala Mkazi wa Kijiwesamli wilaya ya Ilala.
Watuhumiwa hao wote
wanashikiliwa na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na gwaride la
utambulisho.
Post a Comment