NI TCRA, yaani Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndio wanaopaswa kujibu swali hili. Si gazeti moja la Kiswahili Jumapili iliyopita, lilichokonoa suala hili? Lilichokonoa, tena sana na kwa kutoa mifano kama si ushuhuda! Lilianza kwa kumtaja mwandishi wa habari mahiri na mkongwe nchini, ambaye wakati fulani alijifanya mwanasiasa, hatimaye akafanikiwa kuukwaa ubunge, akawa Mbunge wa Muleba Kaskazini kabla ya kurudi kwenye uhalisia wake – uandishi wa habari.
Huyu simwingine bali ni Ndimara Tegambwage ambaye gazeti tajwa hapo juu lilisema kuwa huko nyuma aliwaandikia Watanzania kuwa hataki mpango wa kusajili wamiliki wa simu za mkononi na namba zao kama Serikali ilivyokuwa imeshinikiza.
Likimnukuu Ndimara, liliandika kuwa sababu zilizotajwa na Serikali kuhalalisha usajili na baadaye kusisitizwa na TCRA, kwamba hazikuwa za msingi na hazikuwa na mashiko!
Gazeti hili bwana lina vituko, hasa kwa kupenda kuchokonoa TCRA na Serikali pia! Eti kwa wakati ule watu walifikiri ni ndoto, kwamba Ndimara alikuwa analeta utani na kukejeli ukuaji wa teknolojia!
Eh bwana wee, gazeti hili, eti lilitukumbusha pia kuwa mbuzi dume hapigi chafya bure, na pia kwamba ukimwona nyani mzee, ujue amekwepa mishale mingi! Ni misemo hiyo yenye kutoa ujumbe, upo hapo? Mbuzi dume na nyani mzee ni yupi sasa? Eh!
Eti tulitanabaishwa kuwa Serikali ilibaini wakati huo kuwa simu za mkononi zilikuwa zinatumiwa vibaya, kwamba zilikuwa zinatumiwa kufanya uhalifu. Kwamba zilikuwa zinarahisisha mawasiliano ya wale waliokuwa wanapanga uhalifu!
Eti Serikali yetu haikuwa na hata tone la aibu, ikaenda mbele zaidi na kutaja na kutoa mifano ya uhalifu utakaodhibitiwa baada ya simu kusajiliwa, kwamba ni pamoja na kutukana kupitia kwenye simu za viganjani, kupanga wizi na/au hujuma, kutoa vitisho kwa watu mbalimbali, kutoa taarifa za upotoshaji, n.k.
Gazeti tajwa ‘halikukopesha’ bwana! Liliuliza pasi kusita, miongoni mwa mambo mengine, kwamba sasa baada ya usajili husika, Serikali ituambie imeshindwa nini kupata mtu aliyetekeleza uhalifu wa kutesa, kumpiga na hatimaye kumng’oa kucha Dk. Steven Ulimboka!
Eti ituambie kwa nini wananchi bado wanatishiwa kuuawa, lakini uchunguzi wa polisi unachukua muda mrefu mno! Eti kwa nini uhalifu kwa njia za mitandano unazidi?
Eti Ndimara, ambaye sasa kwa umri wake yuko katika rika la wazee, alitabiri kwamba kwa kusajili simu, Serikali na wenye makampuni ya kutoa huduma za simu za mkononi, walikuwa wamekula njama. Huo ni utabiri, kwamba walikubaliana kuingilia mawasiliano ya wananchi na labda wamekuwa wakifanya hivyo, tena kwa kiwango kikubwa!
Eti ilidhaniwa kuwa ni utani, lakini gazeti tajwa lilitabanaisha wiki hiyo hiyo (iliyopita) lilipotoka kuwa katika kipindi cha “Tuongee” kinachorushwa na Star Tv, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa Serikali, William Lukuvi, alimtishia mtazamaji wa Star Tv, na kusema kuwa anaamrisha wafanyakazi wa ofisini kwake wachunguze kama aliyepiga simu alikuwa Godbless Lema na kudanganya kuwa ni mkazi wa Dodoma!
Eti katika mazingira ambayo waliopewa jukumu la kuzuia uhalifu ndio wenyewe wanaodaiwa kufanya uhalifu, tufanye nini hapa? Pale penye uhalifu unaotiliwa shaka kufanywa na watawala na wateule wao, unahitajika mwarobaini upi kutibu tatizo hili? Wabunge wanaodaiwa kutoa na kupokea rushwa, tena kwa mitandao ya simu zao huku Serikali ipo, sasa inazuia uhalifu upi?
Eti askari polisi wanapodaiwa kushiriki kuiba au kuandaa njama nyingi, tena kwa simu zao, na Serikali ipo kimya, nani atapiga kelele?
Katika mazingira ambayo aliyeibua uhalifu anatendewa kama mhalifu, na wakati mwingine jina lake kuwekwa wazi kwa wahalifu – wawe wakwapuzi wa mabilioni benki, wauza dawa za kulevya au majambazi waliokubuhu – hapa tuko wapi?
Eti tuulize kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ni kesi ngapi leo zipo katika vituo vyote vya polisi - za watu kutishiwa kuuawa kwa njia ya simu? Waliotishwa wapo, waliotishiwa wapo, simu zimesajiliwa, na waliosajili ili wapunguze uhalifu nao wapo!
Kweli gazeti tajwa limesaidia kulonga, kwamba huu ndio ulikuwa ushauri wa Ndimara, kwamba kwa nini hutukumuunga mkono wakati ule?

on Thursday, January 3, 2013
Post a Comment