Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHOW YA DIAMOND PLATINUM YA MAISHA CLUB ILIGUBIKWA NA FUJO TELE

 

Watu Wakiingia Maisha Jana
Juzi Usiku ndani ya maisha club palikuwa na show kubwa ya Usiku Wa Wasafi ila haikwenda kama ilivyo pangwa na msafi Diamond.Watu waliingia club hio mapema na tayari kwa show kali kutoka kwa Diamond. Show ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza, Kundi kubwa la vijana wasiojulikana walianzan kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond. Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi Bestizo Mkononi.Bestizo ni Camera Men na Social Media Personal Wa Diamond kupitia Thisisdiamond.com. Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.
Diamond akiwa jukuwani na jasho likimtoka,kwa mabishano hayo.




Wafanya kazi wa Maisha club wakisafisha Steji baada ya mashabiki kutupa chupa wakati Diamond akiimba.


Chid Benz aliongea na watu na kusema sio kitu kizuri kufanya fujo kwenye onyesho la msanii kama Diamond.Kwani kama una chuki na Diamond mfate mtaani na sio kwenye show yake kwani unaweza kuleta matatizo kwa mashabiki wasio na hatia. Pia Chid Benz alimtuliza Diamond na kumuomba apande kwenye stage kumaliza show na kuburudisha fans waliolipa na kuja kumuona mtu wao.

Vitu vya thamani kama Cheni,Pete na Camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na Uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond Kuharibika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top