MANISPAA
ya Kinondoni imeahidi kuongeza nguvu katika kushughulikia masula ya migogoro
ya ardhi , huku pia ikiwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika mapambano
dhidi ya watu wote wanaokwenda kinyume na utaratibu uliopo.Akizungumza
na jiji Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema
alisisitiza kuwa katika kukabiliana na migogoro hiyo, uongozi wa manispaa
umekuwa ukichukua hatua za haraka kuhakikisha viongozi na watendaji
wanaojihusisha na migogoro na kashfa za ardhi wanachukuliwa hatua mara
moja.
Alisema katika
kuishughulikia migogoro hiyo, manispaa imekuwa ikiendelea kuyafanyia kazi
mapendekezo ya Kamati ya migogoro ya ardhi iliyoundwa kwa maelekezo ya Rais,
hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa imeweza kuleta
mafanikio.
“Hadi sasa migogoro
iliyokuwepo imeshughulikiwa kwa asimilia 95 na kupatiwa ufumbuzi, kwa sasa
migogoro iliyopo ni ile inayotokana na uvamizi wa ardhi unaofanywa na makundi ya
watu kinyjme na sheria ambayo manispaa kwa kushirikiana na Serikali kuu
imeendelea kuipatia ufumbuzi” alisema Fwema.
Aidha alisema kumekuwa na
mawazo potofu ya baadhi ya watu kwamba manispaa hiyo imekuwa ikifanya upendeleo
kwa wakubwa wakati wa uuzaji wa viwanja vyake, madai aliyosema kuwa si ya kweli
na zaidi yamelenga kuichafua manispaa hiyo.
“Madai haya si ya kweli
ikizingatiwa kuwa katika kipindi kinachokaribia miaka 10 manispaa ya Kinondoni
haijawahi kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi kutokana na changamoto
mbalimbali hasa zinazohusiana na utwaaji wa ardhi na ukosefu wa fedha kwa ajili
ya kugharamia fidia na upimaji” alisema Fwema.
Alisema manispaa kwa muda
mrefu imekuwa ikihangaika kutafuta fedha za kupimia viwanja kutoka sehemu
mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha na madhumuni ni kuvipima viwanja hivyo ili
kukabiliana na ongezeko la ujenzi holela katika maeneo
yasiyopangwa.
Kuhusu utoaji wa vibali vya
ujenzi na kushughulikia maombi ya kubadili matumizi ya ardhi, Fwema alisema
manispaa hiyo kwa kutumia wataalam wake, kabla ya kutoa vibali hivyo wameweka
utaratibu wa kuhakikisha maombi yaliyotolewa, hayakinzani na matumizi yaliyopo
na yaliyoidhinishwa katika mpango wa matumizi ya ardh
Post a Comment