MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (Ewura) imesema kuwa haitakurupuka kutangaza bei mpya ya umeme, badala yake kwa sasa inafanya tathmini na kukusanya maoni ya wananchi, wadau na Serikali kabla ya kupandisha bei ya umeme.
Pia Mamlaka hiyo imesema bei halisi itatangazwa Januari mwakani, endapo Serikali itashindwa kutoa pesa kwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Pia Mamlaka hiyo imesema bei halisi itatangazwa Januari mwakani, endapo Serikali itashindwa kutoa pesa kwa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo, Titus Kaguo alisema kwa sasa mamlaka hiyo inaendelea na mchakato wa kufuatilia na kukusanya maoni ya wananchi, wadau wa nishati hiyo pamoja na Serikali kabla ya kutoa tamko la kupandishwa kwa gharama za umeme.
“Bei halisi itatangazwa Januari mwakani ila kwa sasa Ewura inaendelea na mchakato wa kufuatilia maoni ya wadau, wananchi na Serikali ili kujua kama tunaweza kupandisha bei iwapo Serikali haijatoa fedha kwa Tanesco,” alisema.
Alisema kuwa mchakato wa kutangazwa kwa bei mpya huwa ni siku 81, hivyo hawawezi kutangaza bei mpya ya umeme wakati hawajafanya tathmini ya maoni ya wananchi, wadau na Serikali.
Alisema kama Serikali itaipatia fedha Tanesco, Ewura itazifanyia tathmini na kujua ni kiasi gani kimepatikana kama kinakidhi mahitaji ya umeme.
Awali, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), liliomba kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 81.27 kutoka Sh196 ya sasa hadi Sh359 kwa uniti moja ya umeme ili litoe huduma bora za upatikanaji wake.
Awali, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), liliomba kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 81.27 kutoka Sh196 ya sasa hadi Sh359 kwa uniti moja ya umeme ili litoe huduma bora za upatikanaji wake.
Hata hivyo, Ewura ilipandisha gharama hizo kwa asilimia 40.29, licha ya kuwa bei hiyo ilikuwa iwe kwa miezi sita.
Pamoja na Tanesco kuomba kupandisha gharama za umeme, Serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ilisema bei ya umeme haitapanda kama Tanesco ilivyopendekeza.
Alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha yanaenda sambamba na kutafuta kampuni nyingine za kuzalisha umeme nchini ili kuboresha huduma hiyo kwa wateja.
Waziri huyo alisema mapendekezo ya Tanesco kupandisha gharama za umeme na ambayo Ewura iliyapokea, hayalengi kutatua matatizo ya shirika hilo.
Waziri huyo alisema mapendekezo ya Tanesco kupandisha gharama za umeme na ambayo Ewura iliyapokea, hayalengi kutatua matatizo ya shirika hilo.
Alisema kuwa tatizo ndani ya Tanesco siyo pesa bali ni mfumo mbovu wa uendeshaji, ambao unalifanya shirika hilo kuwa mzigo na kushindwa kutoa huduma bora kwa wateja wake, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wateja.
Alisema msimamo wa Serikali ni kwamba haitapandisha bei gharama za umeme kutoka na Tanesco kuwa na mfumo mbovu.
Alisema kwa sasa wapo mbioni kuifumua Tanesco na kuangalia uwezekano wa kupata kampuni zaidi ya mbili za kuzalisha umeme kutokana na mfumo wa menejimenti uliopo kuwa ni mbovu na umepitwa na wakati.
Profesa Muhongo alisema kuanzia Januari mwakani watabadilisha muundo huo ili kupata kampuni ya kuzalisha na ya kusambaza umeme nchini na kwamba baada ya mabadiliko hayo Tanesco inaweza kutoa maoni ya kuomba kuongeza gharama za nishati hiyo.
Post a Comment