Akizungumza baada ya wabunge kuupitisha mswada huo Rais
Obama alisema kuwa kura za wabunge zimeuepusha mchanganyiko wa kupandisha kodi
mara moja, na kukata matumizi ya mfuko wa kijamii, mchanganyiko ambao
ungeliirudisha Marekani katika mshuko mwingine wa uchumi. Hata hivyo amekiri
kwamba nakisi katika bajeti ya Marekani bado ni kubwa
sana.
Obama ameeleza kwamba Marekani bado inawekeza kidogo
kwa ajili ya yale yanayohitajika kufanyika ili kuustawisha uchumi haraka.
Amesema Wamerakani hawawezi kutumia njia ya mkato ili kufikia kwenye neema
.
Obama ameeleza kuwa anakubaliana na wajumbe wa
Republican na Democrats kwamba nakisi lazima ipunguzwe. Lakini amesema kupunguza
nakisi lazima kuende sambambana mageuzi katika mfumo wa kodi. Amesisitiza kuwa
ni lazima Marekani isonge mbele katika kupunguza nakisi, lakini kwa
wizani"
Rais Obama aliekatiza mapumziko yake huko Hawaii ili
kurejea Washington kuhimiza kufikiwa kwa suluhisho la bajeti atautia saini
mswada huo ili uwe sheria. Lakini amesisitiza kuwa harakati za kupambana na
nakisi zitaendelea.
Deni la Marekani limekuwa linaongezeka katika kipindi
cha miaka10 iliyopita na kufikia dola Trilioni 16 sasa. Sababu kadhaa
zimeisababisha nakisi hiyo kubwa, ikiwa pamoja na, hatua iliyochukuliwa na
utawala wa George Bush ya kupunguza kodi. Vita vya Iraq na Afghanistan, mshuko
wa uchumi na mgogoro wa fedha pia ni sababu zilizochangia katika kuiongeza
nakisi hiyo.
Mswada uliopendekezwa na Seneti na kuridhiwa na Baraza
la wawakilishi utazuia kupandishwa kodi kwa Wamarekani wote na utaepusha kukatwa
kwa mfuko wa matumizi. Badala yake kodi zitapandishwa kwa familia zenye mapato
yanayovuka dola laki nne kwa mwaka. Kodi kwa familia hizo zitapanda kwa asilimia
39.6 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 35. Kupandishwa kodi kwa familia hizo
kutaingiza mapato ya dola Bilioni 620 katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Mswada huo pia utawezesha kuurefusha kwa mwaka mmoja, muda wa kuwalipa
Wamarekani milioni mbili wasiokuwa na ajira.
Hatua ya kukata matumizi itaahirishwa kwa muda wa miezi
miwili wakati bunge linatafakari mpango mbadala. Wabunge 257 walipiga kura ya
ndio kuipitisha rasimu hiyo na167 waliipinga. Kura zilipigwa saa 24 tu baada ya
Seneti kuipitisha rasimu hiyo ambapo masenata 89 waliiunga mkono na wengine
wanane waliipinga.
Post a Comment