Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akiwakagua wachezaji wa timu ya Mikocheni Warriors na wachezaji wa timu ya Kawe Kombaini wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Meya, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akimwongoza Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk Fenella Mukangara
(katikati), Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus
Fwema na viongozi wengine mara baada ya ukaguzi wa
timu
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni,
Yusuph Mwenda akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa michuano
hiyo
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara (kulia)
akibadilishana mawazo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa
ufunguzi wa michuano ya kombe la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki
Mshambuliaji
wa Kawe Kombaini, Hassan Ngonyani (kulia)
akitafuta
mbinu za kumtoka beki Ally Ramadhan
wa Mikocheni Warriors wakati wa mechi ya ufunguzi ya
Kombe
la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kawe
walishinda kwa
magoli 3-1.
Golikipa
wa Kawe Kombaini Simon Adamu akiudaka mpira huku wachezaji wa timu ya Mikochezni
Warriors wakijiandaa kupiga
goli. Kawe ilishinda magoli 3-1.
Post a Comment