Wanachama wa timu ya Yanga
kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa
Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano
wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo
uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa
Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu
hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini katika
mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao
3-2.
Mwenyekiti Mpya wa Club ya
Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano
huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo
yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo
ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya
yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na
wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
Sehemu ya meza kuu ya
mkutano huo ilivyokuwa.
Makamu mwenyekiti wa timu
ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe
wa mkutano huo.
Pichani kulia ni mchezaji
wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa
Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa
muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya
shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
Pichani juu na chini ni
baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya kuuliza maswali
mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali
waliohudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf
Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement Sanga wakifatilia jambo
kwa makini ukumbini humo.
Pichani baadhi ya
wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati
mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
Baadhi ya Wazee wa baraza
wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo
mkuu wa Kihistoria.
Kocha mpya wa timu ya
Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache
kuhusina na timu yake ya Yanga.
Pichani ni baadhi ya
Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo
uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam
mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya
leo.
Msanii mahiri wa kizazi
kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano
huo.
Mtangazaji machachari wa
kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa
Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa
Mwaka.
Post a Comment