Wananchi wakisubiri kwa hamu kuanza kwa mashindano ya resi za ngarawa yalioyofanyika huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wananchi wakishangilia jinsi mpambano ulivyokuwa mkali huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ngarawa mbili za mbele zikichuana vikali katika mashindano yalio fanyika huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mshindano hayo Nahodha Fundi Abuubakar kutoka Bumbwini.