Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akitia saini Mpira katika uzinduzi wa
Mradi
wa ”ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA”,mradi ambao utawapatia
vijana
wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu ,(20,000) katika vikundi mbali
mbali
na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka nchini,katika sherhe
za
kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na
Ramadhan
Othman,Ikulu.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohammed Shein ameuagiza uongozi wa
Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Amali kuhakikisha michezo yote inayoruhusiwa
kisheria Zanzibar kuchezwa mashuleni isipokuwa mchezo wa Ngumi
(Boxing).
Amesema michezo yote
inafaa kuchezwa wala haipunguzi kasi ya mwanafunzi kusoma na kwamba Wizara
inapaswa kulisimamia agizo hilo ili Zanzibar iweze kupata vipaji vitakavoiletea
nchi Medali za mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Rais Shein ameyasema
hayo alipokuwa akizindua Mradi wa “Mpira Mmoja” “One World Football ball Project
for Africa” Wenye lengo la kupambana na Ukatili dhidi ya Watoto kupitia mchezo
wa Mpira katika Uwanja wa Aman mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49
ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema Mradi huo ambao
umewalenga zaidi Wanafunzi wa Shule umefufua matumaini mapya ya kuibua vipaji
vya michezo mbalimbali Zanzibar na kwamba kinachohitajika kwa sasa ni mipangilio
mizuri kutoka kwa Walimu na wasimamizi wa michezo
mashuleni.
Aidha amesisitiza kuwa
michezo haimzuii mwanafunzi kufanya vizuri darasani hivyo Wazazi na walezi
waendelee kutoa mashirikiano kwa watoto wao kuhusu michezo stahiki
wanayoipenda.
“Jukumu lenu Wizara ya
Elimu ni kuhakikisha kuwa Michezo yote ile iliyoruhusiwa kisheria chini ya
Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo kuwa inachezwa Mashuleni..Wala
michezo haimzuii mwanafunzi kufanya vyema Darasani ” Alisema Rais
Shein.
Rais Shein alifahamisha
kuwa mradi huo pia utasaidia sana kujenga kikosi imara cha Timu ya Taifa ya
Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa vile vipaji vya Soka vitaibuka vingi mashuleni
vitakavyosaidia Timu hiyo kuwa tishio Afrika Mashariki na
Kati.
Akigusia suala la
Zanzibar Heroes na ushindi wa nafasi ya tatu uliyoipata katika Mashindano ya
SECAFA Rais Shein amesema timu hiyo ilicheza vizuri kiasi cha kumvutia sana na
kuongeza kuwa Zawadi yao ipo kinachohitajika ni kumalizwa tofauti baina ya
Wachezaji na Viongozi wa Timu hiyo.
Kwa upande wake Waziri
wa Habari na Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Mradi huo
umelenga kuleta vuguvugu la michezo na kuondoa tatizo la vifaa vya michezo
Zanzibar ili kuibua vipaji vitakavyoifanya Zanzibar iwe tishio katika michezo
mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa
Mipira hiyo itagaiwa katika maeneo yote ya Unguja na Pemba bila ya upendeleo na
kwamba Timu zote zilizosajiliwa na Makundi maalum watanufaika na mipira
hiyo.
Mradi huo ambao
umefadhiliwa na One World Futbal,Shirika la Kusaidia Watoto Duniani kwa
kushirikiana na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar unajumuisha Mipira-Elfu 20,
itakayogaiwa kwa Wanafunzi wa shule na Timu za Soka za Unguja na
Pemba.
Post a Comment