Wachezaji wa Yanga wakishuka kwenda uwanja wa
mazoezini jioni ya jana. |
Dah... huku kunatamanisha sana kubaki! Kutoka
kushoto ni Nadir Haroub 'Cannavaro', Frank Domayo na Simon Msuva. Hapa wakipozi kwa picha wakati wa
mazoezi ya timu yao ya Yanga nchini Uturuki jana Desemba 31,
2012. |
|
Hoteli
walilofikia Yanga nchini Uturuki... ni maraha
utamu! |
|
Simba
watatukoma mwaka huu... makocha wa Yanga, Razak Siwa (kushoto) na Ernst Brandts
wakitafakari wakati vijana wao (hawapo pichani) wakiendelea kujifua jana Desemba
31, 2012. |
|
Huku
tukizubaa lazima tuwe masharo kwa sana... Cannavaro (kulia) na Razak Khalfan wa
Yanga wakiwa kwenye uwanja wao wa mazoezi nchini Uturuki jana Desemba 31,
2012.
|
Magolikipa
Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul wakiwa katika mazoezi ya
asubuhi leo nchini Uturuki |
Wachezaji wa Young Africans
wakiwa katika mazoezi ya asubuhi leo hii - Antalya Uturuki
Wachezaji na bechi la
ufundi la timu ya Young Africans wamefurahishwa na hali ya kambi hapa katika mji
wa Antalya kwamba hali ya hewa ni nzuri, vyakula aina zote vinapatiikana na
huduma za mazoezi kwa ajili ya kambi ni za kiwango cha juu
sana.
Wakiongea na
www.youngafricans.co.tz Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli hali ya
hewa sio mbaya kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya hewa ni nzuri,
mazingira ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili ya mazoezi vipo kwa
wingi hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu kuwaelekeza wachezaji wafanye
nini.
Kocha Siwa amesema pia
wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua kuileta timu kambini nchini
Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo
ambayo hayana bughuza kwani kambi ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu
nyingi za Ulaya
Wachezaji wa Young Africans
wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Fame Residence Analya -
Uturuki
zinapenda kuja kuweka
kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.
Fred Felix Minizro kocha
msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa ujumla ni nzuri, na kuhusu
hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya na Arusha hivyo haoni kama hali ya
hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika kambi hii ya mafunzo.
Naye kiungo mshambuliaji
Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii ya kuja kuweka kambi nchini
Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z akambi ni nzuri kabisa hivyo
wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu Brandts na pindi watakaporudi Tanzania
wataweza kuwapa raha wapenzi wa soka kwa kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa
kipindi cha wiki mbili
|
on Wednesday, January 2, 2013
Post a Comment