Usaili
na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Ramadhan Dau, mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa
wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alisema mfuko huo utawekeza shilingi milioni 500
(dola 32,000) katika mpira wa miguu mwaka ujao.
Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Ramadhan Dau akihutubia wahariri katika
hoteli ya Sea Cliff huko Zanzibar tarehe 3 Disemba, 2012. [Deodatus
Balile/Sabahi]
Dau alisema kampuni hii ya dola, ambayo inasimamia pensheni za wafanyakazi wa Tanzania, mwanzoni iliwekeza katika soko la mali isiyohamishika ili kuendeleza mtiririko wake wa fedha, lakini kufuatia tathmini yakinifu ya hivi karibuni bodi ya kusimamia shughuli za utawala iliamua badala yake kuwekeza katika mpira wa miguu.
Dau alisema kampuni hii ya dola, ambayo inasimamia pensheni za wafanyakazi wa Tanzania, mwanzoni iliwekeza katika soko la mali isiyohamishika ili kuendeleza mtiririko wake wa fedha, lakini kufuatia tathmini yakinifu ya hivi karibuni bodi ya kusimamia shughuli za utawala iliamua badala yake kuwekeza katika mpira wa miguu.
Uwekezaji wa mwaka ujao utakua wa kuanzia wa
kile ambacho Dau aliita chombo cha uwekezaji wa muda mrefu kwa NSSF ambacho
kitasaidia kutoa ajira na mapato kwa wachangiaji wa mfuko
Dau, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
na aliyejieleza kuwa shabiki wa mpira wa miguu, alikaa pamoja na Sabahi kujadili
ni kwa nini NSSF iliona ni lazima kuwekeza katika mpira wa miguu na ni kwa namna
gani inapanga kufanya mradi huo kuwa wa faida kwa wachangiaji.
Sabahi: Watanzania wanapenda mpira wa miguu,
lakini nchi imeendelea kuwa na hali duni katika mashindano ya kimataifa. Nini
kitafanyika kuinua viwango vya mpira wa miguu?
Ramadhan Dau: Tunao vijana wenye afya na
vipaji. Mpira wa miguu ni mchezo wa kwanza katika nchi kwa idadi ya mashabiki.
Mashabiki wako tayari kuchangia fedha za kiingilio hata kwa matokeo mabaya.
Nilishangaa ni nini tunachokikosa kama nchi na jibu liko wazi. Tunakosa
usimamizi imara wa mpira wa miguu.
Sabahi: Ni nini ambacho NSSF inapanga kufanya
kuhusiana na hilo?
Dau: Katika mkutano wa mwisho wa bodi ya NSSF
[uliofanyika mwezi Disemba], tulikubaliana kwamba hatuwezi kuendelea kubakia
kuwa watazamaji. Kama shirika lililopo la kujenga matumaini, tuliamua kuwekeza
kwa kiwango kikubwa katika mpira wa miguu. Tumetenga shilingi za Kitanzania
milioni 500 (dola 32,000) katika bajeti ya 2013 kuwekeza katika mpira wa
miguu.
Mwezi Oktoba uliopita, nilisafiri kwenda
Manchester nchini Uingereza kuweka mipango kwa ajili ya jambo hili. Tunataka
kuingia katika mkataba na timu zenye viwango katika dunia ili kunufaika na
msaada wao wa kiufundi katika jitihada zetu za kuhuisha mpira wa miguu
Tanzania.
Kwa kuanzia, tutaandikisha watoto [wenye umri
wa miaka 7 hadi13]. Watapewa mafunzo yenye viwango ambayo yatajumuisha mafunzo
ya kimwili na kisaikolojia yakilenga kuwafanya kuwa wachezaji wazuri wa mpira wa
miguu. Tutaajiri madaktari kuwahudumia na kutoa mlo kamili kudumisha afya imara.
Vijana hawa, wachezaji wenye vipaji watakwenda shule asubuhi na kurudi [katika
kambi] jioni kwa mafunzo ya mpira wa miguu.
Sabahi: Uliposafiri kwenda Uingereza ulipata
mwitiko gani kwa watu wa kule?
Dau: Majibu yao yalikuwa mazuri sana.
Nilikutana na [meneja wa Manchester United] Sir Alex Ferguson ambaye alivutiwa
sana na mpango huu. Kadri itakavyoendelea, ushirikiano wao [na timu za
kimataifa] utaendelea kupanuka zaidi kuliko [kutoa msaada wa kiufundi]. NSSF
itawalea wachezaji hawa vijana hadi umri wa mika 15 na 17, kisha [itawasaidia
kutafuta mikataba na] vilabu vikubwa kutoka Ulaya au katika nchi nyingine
zinazowataka duniani.
Nilikuwa nimesema kwamba tatizo kubwa kwa mpira
wetu wa miguu ni usimamizi. Tunataka kuondoa tatizo hilo. Baada ya kuwachagua
vijana wadogo [wenye vipaji], tutaingia nao mkataba [kwa kupata idhini] ya
wazazi wao.
Tutawalipa mishahara ya kila mwezi na fedha
hizo zitakwenda moja kwa moja katika akaunti zao binafsi za benki. Fedha hizo
zitakuwepo [kwa matumizi yao binafsi] wakati NSSF italipia gharama za kujikimu
na ada ya shule wakati wote wa kipindi cha mkataba.
Mkataba utaiwezesha NSSF kurejesha gharama za
kuwekeza pale mchezaji anapouzwa nchi za nje. Hii ina maana tutatoa wachezaji
bora wenye uwezo wa kurejesha malipo ya gharama zilizotumika kuwekeza. Kwa
mfano, kama tutatumia kiasi cha dola milioni 1 hadi milioni 3 kwa kipindi cha
miaka tano hadi nane kumpa mafunzo mchezaji, na kuweza kumuuza mchezaji kwenye
vilabu vyenye hadhi duniani kwa kiasi kama cha dola milioni 8, hii ina maana
tutarejesha gharama na kugawana faida. Kwa namna hiyo tutadumisha mradi
huo.
Sabahi: Hatua inayofuatia katika mpango ni
ipi?
Dau: Dira ni kujenga chuo cha mpira wa miguu,
lakini hatutaki kusubiri. Mwanzoni mwa mwaka ujao, tutakodi jengo na kulifanya
kuwa [bweni]. Wachezaji hao vijana wenye vipaji wataendelea kwenda shule katika
shule za umma wakati tunakamilisha mchakato wa kujenga chuo katika vitongoji vya
Dar es Salaam.
Sabahi: Mtaajiri wachezaji wangapi na vigezo
vitakuwa ni vipi?
Dau: Tumepanga bajeti ya wachezaji 50 kwa mwaka
2013. Lakini kadri tunavyoendelea, idadi itaongezeka kufikia kiasi cha 300. Hiyo
ndiyo shabaha yetu katika miaka kumi ijayo. Tutatumia mashindano baina ya shule
[kuchagua wanafunzi]. Kutoka shule ya awali, tutaanza kutambua vipaji vya
wanafunzi nchi nzima na kuviendeleza.
Sabahi: Suala hilo litainufaishaje nchi na
kusaidia kuboresha mpira wa miguu?
Dau: Hilo liko wazi. Kwanza kabisa, [ NSSF]
itakuwa na klabu ya mpira wa miguu ambayo itashiriki katika ligi yetu kuu ya
taifa. Kwa kuwa na wachezaji waliyomotishwa ambao wamepata mafunzo mazuri na
wanaolipwa vizuri, nina uhakika watainua kiwango cha ligi kuu.
Sabahi: Mwezi Disemba, FIFA, shirika la
kimataifa ambalo linasimamia mpira wa miguu na kuandaa Kombe la Dunia, liliiweka
Tanzania katika nafasi ya 130 kati ya wanachama 207. Tanzania itafikia nafasi ya
ngapi kwa uwekezaji wa NSSF?
Dau: Lengo letu la kwanza ni kuwa nafasi 50
bora. [Baada ya hapo], tutajitahidi kuwa katika nchi 30 bora na kuendelea
kupanda juu, tukidhamiria namba moja. Sioni ni kwa nini tusiweze.
Sabahi: Lengo kubwa zaidi la NSSF katika
programu hii ni lipi?
Dau: Ushiriki wetu wa kwanza na pekee katika
Kombe la Mataifa ya Afrika ilikuwa mwaka 1980. Hatujawahi kamwe kushiriki katika
Kombe la Dunia kama nchi. Sasa tunapaswa kufika huko. Tumesubiri kwa muda mrefu
na NSSF inaahidi kubadilisha hali hii isiyokubalika.
Post a Comment