Naibu Waziri wa TAMISEMI
Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa moja ya barabara zilizojengwa
na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo kuhakikisha kama barabara hiyo
imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu
Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema
fedha za Serikali katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha
zilizotumika, alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali
katika mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani
Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI
Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo chini ya Halmashauri ya
Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi karibuni. Katika ukaguzi huo alibaini
mapungufu mbalimbali katika ujenzi huo na kuagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha
mapungufu hayo yanaondolewa. Aliitaka pia halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi
za Serikali kuepusha minong’ono inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu wa
baadhi ya watendaji Serikalini.
Mhe. Agrey Mwanri akiweka
jiwe la msingi kiwanda cha unga cha Malangali kinachomilikiwa na muwekezaji wa
ndani mapema hivi leo. Kwa sasa Mkoa wa Rukwa una viwanda vitatu vya unga
vinavyomiliwa na wawekezaji wa ndani.
Naibu wa Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Agrey Mwanri
akikagua kiwanda cha unga cha Malangali Mjini Sumbawanga leo alipotembelea
kiwandani hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la
msingi.
Mhe. Mwanri akizungumza na
wakazi wa Mji wa Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi ya Mjini hapo ambapo
alipokea kero mbalimbali ikiwepo ubovu wa miundombinu ya umeme na barabara
katika stendi hiyo. Aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya Mkutano
wa hadhara na wananchi hao kuskiliza kero zao zote pamoja na kuzitaftia ufumbuzi
na kumpelekea taarifa ya utekelezaji.
Katika
hali isiyotegemewa msafara wa Mhe. Mwanri ulipowasili katika kijiji cha Mlanda
katika Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya Mkutano wa hadhara ulikuta msiba
ambapo walishiriki na kutoa ubani ambapo Mhe. Mwanri alitoa laki moja na alfu
mbili na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini CCM ambaye pia ni Mjumbe wa
halmashauri kuu Taifa ya CCM (NEC) kupitia
Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal alikabidhi shilingi alfu
hamsini.
Post a Comment