Kikosi cha Tusker leo |
Na Mahmoud
Zubeiry, Zanzibar
TUSKER FC
imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu baada ya kuifunga
Miembeni FC ya hapa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Kwa ushindi
huo, Tusker itamenyana na Azam katika fainali ya michuano hiyo keshokutwa kwenye
Uwanja wa huu huu wa Amaan.
Hadi
mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na zote
zilishambuliana kwa zamu na kila timu ilipoteza nafasi mbili za wazi za kufunga
mabao.
Lakini
kipindi cha pili Tusker walirekebisha makosa yao na kufanikiwa kupata mabao
yaliyowavusha Fainali ya michuano hii.
Bao la
kwanza alifunga Luke Ochieng dakika ya 52 kabla ya Jesse Were kufunga la pili
dakika ya 72, ambalo linakuwa bao lake la nne katika mashindano
haya.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Miembeni FC kilikuwa; Abdulsamad Sele, Kassim Hamad,
Adeyum Saleh, Salum Hajji, Ibrahim Abbas, Sabri Ally, Suleiman Ali/Omar Tamim dk
83, Laurent Mugia/Salim Seif ‘Bakayoko’ dk83, Monja Liseki ‘Anelka’/Peter Ilunda
dk 10, Rashid Roshwa/Mohamed Salum dk58 na Issa Othman
‘Amasha’.
Tusker FC;
Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Bright Jeremiah, Mark Odhiambo, Martin
Kizza/Humphrey Okoth dk89, Frederick Onyango, Justine Monga/Andrew Tololwa dk54,
Khalid Aucho, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk73, Ismail Dunga na Robert
Omonok.
Post a Comment