![](https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn1/75556_396685527080537_1721058596_n.jpg)
MWANDISHI wa Habari wa
kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa Ngumba (45) ameua
kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na
Bastora iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake
porini.
Habari ambazo
zimepatikana na kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na
kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu
ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo imedai mwandishi huyo amekutwa
ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu ambao hawajajulikana.
Akizungumza na gazeti
hili jana kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa
waliwasiliana na waandishi wa wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la
tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus Ijumaa aliyeeleza kuwa mwili wa
marehemu umenyongwa ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi mkono wa
kushoto.
Mwili wake umepatikana
jana katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya
asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea Jumapili siku moja
baada ya kutoonekana kwake.
“Sisi tunaelekea wilaya
ya Kakonko toka Kigoma mjini, lakini walioshuhudia mwili huo huko eneo la tukio
waneleza kwamba kando ya mwili wake kumekutwa Bastora moja, haijafahamika iwapo
ilikuwa inamilikiwa na marehemu ama nani, simu zake mbili na kwa mujibu wa
Dkatari maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi,” alieleza
Sonkolo.
Imeelezwa kwamba bastora
iliyokutwa eneo la tukio imekutwa na ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali
ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.
Kwa upande wake kamanda
wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo
lakini alisema kwa sasa jeshi lake linangoja taarifa ya daktari aliyefanya
uchunguzi wa mwili wake ikiwa ni pamoja na taarifa ya awali ya uchunguzi wa
jeshi hilo toka eneo la tukio.
Aidha akizungumza na
gazeti hili Naibu Mharari wa kituo cha Radio Kwizera kinachorusha matangazo
kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu, alisema kwamba tokea Januari 5
mwaka huu walikuwa majira ya saa 11 walikuwa wakijaribu kuwasiliana naye na simu
zake zilikuwa zikiita bila ya kupokelewa mpaka jana ambapo zilikuwa
hazipatikani.KATUNI NEWZ
Post a Comment