Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VYAMA VYA CCK, UMD, DP NA AFP NAVYO PIA VYATOA MAONI YAO MBELE YA TUME YA KATIBA

Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constantine Makitanda akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mara baada ya Chama hicho kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (Jumanne Januari 8, 2013).
Katibu wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD),Ndg. Juma akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika leo (Jumanne Januari 8, 2013) baina ya Chama hicho na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambapo Chama hicho kiliwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume,Assaa Rashid.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD) wakifuatilia mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo( Jumanne Januari 8, 2013), ambapo Uongozi wa Chama hicho uliwasilisha maoni ya Chama hicho kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP), Rashidi Mohamed akiwasilisha maoni yao kuhusu Katiba kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo (Jumanne, Januari 8 2013).
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Raza Hamad akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Wakulima (AFP) uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (Jumanne Januari 8, 2013).
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (jumanne Januari 8, 2013).
Mjumbe Wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ndg. Ussi Khamis akizungumza katika mkutano na Viongozi wa Chama cha Kijamii (CCK) uliofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam wakati Chama hicho kilipowasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya leo (jumanne Januari 8, 2013).

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza na Viongozi wa Chama cha Democratic (DP) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) waliofika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo kuwasilisha maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Katikati ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.
Viongozi wa Chama cha Democratic (DP) wakiongoz wa na Mchungaji Christopher Mtikila (kushoto) wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam leo

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (katikati) akizungumza katika mkutano uliofanyika leo katika Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam na Chama hicho kilipowasilisha maoni yao Kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Jaji Joseph Warioba (katikati) ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top