**********
WASISI wa Chadema,Edwin Mtei amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa sasa.
Kauli hiyo ya Mtei inakuja siku kadhaa baada ya
kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba Dk
Slaa awanie tena urais katika uchaguzi ujao huku yeye akijiondoa katika
orodha ya viongozi watakaowania nafasi hiyo kupitia Chadema.
Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto
anapaswa kumwachia Dk Slaa apeperushe bendera ya chama hicho katika
uchaguzi ujao kwa kuwa ndiye chaguo la wengi.
“Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa
amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao
kwani ndiye chaguo la wengi,” alisema Mtei.
Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.
Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.
Alisema kila mmoja ndani ya chama amekuwa na hisia
na mawazo tofauti lakini msimamo wake kwa sasa ni kumtaka Dk Slaa
awanie nafasi hiyo ya urais na si Zitto. “Kila mmoja na hisia na maoni
yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na
Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera,” alisema Mtei.
Hata hivyo, Mtei alisema Zitto ana haki ya
kuonyesha demokrasia yake ndani ya chama kwa kutangaza kuwania uraisi
mwaka 2015 na ndiyo maana halisi ya chama chao.
“Kuonyesha hisia si dhambi, kila mtu ana hisia zake hata yeye (Zitto) ana sababu za kuonyesha hisia zake,” alisema Mtei.
“Kuonyesha hisia si dhambi, kila mtu ana hisia zake hata yeye (Zitto) ana sababu za kuonyesha hisia zake,” alisema Mtei.
Hata hivyo, alionya kuwa kila mmoja mwenye hisia
za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao anapaswa kusubiri mchakato wa
mchujo wa majina utakaofanyika ndani ya chama muda mwafaka ukiwadia.
Post a Comment