Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemteuwa Profesa Ali
Seif Mshimba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango la Zanzibar(Zanzibar
Bureau of Standards) katika Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko
Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa
iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.
Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais amefanya uteuzi huo kwa uwezo aliopewa
chini ya kifungu 8(2)(a) cha Sheria ya Viwango namba 1 ya mwaka
2011.
Uteuzi huo umeanza
jana.
IMETOLEWA NA IDARA YA
HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Post a Comment