Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TFF KUKAA MEZANI NA SIMBA NA YANGA ILI WAWAPE RUHUSA WACHEZAJI WAO KUJIUNGA NA KAMBI YA TAIFA STARS




SHIRIKISHO la soka nchini TFF limesema kuwa litafanya majadiliano na vilabu vya SIMBA na YANGA ambavyo vimetishia kutowaruhusu wachezaji wake kujiunga na kambi ya TAIFA STARS iliyopangwa kuanza JANUARI SITA mwaka huu.

Msemaji wa shirikisho hilo , BONIFACE WAMBURA amesema kambi hiyo ya TAIFA STARS dharura ni ya wiki mbili ambayo itamsaidia kocha KIM PAULSEN kuwafahamu vizuri wachezaji ambao amewaita kutoka katika timu ya KILIMANJARO STARS na wale wa ZANZIBAR HEROES (PAUSE)

Kuwaita wachezaji wa TAIFA STARS ni kutokana na kocha PAULSEN kuanza kufanya matayarisho ya kuikabili vizuri timu ya MOROCCO katika mashindano ya kutafuta kombe la dunia mchezo utakaochezwa mwezi Machi mwaka huu.

Katika kundi la TAIFA STARS kuna timu nyingine za IVORY COAST na GAMBIA.

Katika hatua nyingine , msemaji wa TFF , BONIFACE WAMBURA amesema bado michezo ya kirafiki inatafutwa ili kuiandaa TAIFA STARS na mashindano hayo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana