Makao Mkuu ya NCCR-MAGEUZI
Mbunge
wa Kasuru, Moses Machali (katikati) akizungumza kabla ya kukabidhi kadi
ya uanachama kwa mwanachama mpya aliyejiunga na chama hicho.
Eddo Mkata akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujiunga na NCCR-MAGEUZI.
DAR ES SALAAM. Tanzania
BAADA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumtimuwa uwanachama Edo
Mwamalala, hatimaye mwanachama huyo ametangaza rasmi kujiunga na Chama
cha Mageuzi ya Taifa (NCCR- Mageuzi).
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwamalala, alisema
harakati za kisiasa alizianza tangu akiwa kijana, kuwa muumini wa siasa
za upinzani na rasmi alijiunga na Chadema.
Alisema
ameamua kujiunga na Chama hicho kutokana na ukweli kwamba ndicho chama
kinachoonekana kuwa chama chenye utu, misingi bora ya usawa, uheshimu wa
haki za wanachama na Watanzania pamoja na mshikamano.
“Kwa
furaha kubwa kabisa na penda kuchukua fursa hii kuwatangazia Wanambeya
na umma wa Watanzania kwa kuvunja ukimya na sasa natangaza kujiunga na
chama cha NCCR-Mageuzi na nisema kuwa huu ni mwanzo tu mimi nimetangulia
na wengine watakuja au kufuata hatua kwa hatua”alisema Mwamalala.
Hata
hivyo, Mwamalala alipinga kuwa alifukuzwa chama bali kilichotokea ni
kwamba mwanzoni mwa Januari 3 mwaka huu alitangaza kujiuzulu nafasi zote
za uongozi ndani ya Chadema ikiwa ni pamoja na kujivua uanachama wa
chama hicho.
Pamoja na kudai kuwa hajafukuzwa, taarifa za Chama hicho zinaeleza kuwa Mwamalala alifukuzwa uwanachama tangu mwaka jana.
Post a Comment