Ujenzi
 wa vifaa (turnstiles) vitakavyotumika kwa ajili ya tiketi za 
elektroniki kwenye viwanja saba kati ya nane vitakavyotumia mfumo huo 
umekamilika kwa asilimia 80.
Viwanja
 hivyo ni Chamazi (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba),
 Sokoine (Mbeya), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Mkwakwani 
(Tanga).
Wakati
 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari una turnstiles, Uwanja wa CCM 
Kirumba jijini Mwanza bado haujaruhusu ufungaji wa vifaa ukisubiri 
idhini kutoka kwa wamiliki wake (CCM Makao Makuu).
Vifaa
 vitakavyotumika kusoma tiketi za elektroniki katika viwanja hivyo 
vinatarajiwa kuwa vimefungwa kufikia Februari 20 mwaka huu.
Hakutakuwa
 na matumizi ya fedha taslimu mara baada ya mradi huo wa tiketi la 
elektroniki kuanza, kwani tiketi zitakuwa zikinunuliwa kwa kadi maalumu 
(smart card) katika vituo mbalimbali vitakavyotangazwa baadaye.
Benki
 ya CRDB ndiyo iliyoingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu 
Tanzania (TFF) kutengeneza tiketi za elektroniki baada ya kuibuka 
mshindi kwenye tenda.


Post a Comment